Thursday, April 08, 2010

Mambo ya mashujaa Musica


Salha Salehe

Salha Salehe, Rose, Masaki

Amosi Solo

Elystone Angai

Mariam+Lela+Pee

Bendi Mpya ya Mashujaa Musica ambayo imeundwa mwaka huu na kuweza kufikia mafanikio makubwa kwa muda mfupi hata kufikia kuliteka jiji la Dar es Salaam na Vitongoji vyake baada ya kuteremsha vibao viwili ambavyo mashabiki kote nchini waliobahatika kusikia na kutazama katika televisheni wameweza kushuhudia jinsi bendi hiyo inavyokuja kwa kasi hata kuwaweka roho juu baadhi ya wamiliki wa bendi kubwa zikiwemo za Twanga, Fm Academia na Acudo Impact.

Mashujaa Musica kwa sasa ipo chini ya uongozi wa Elystone Angai anayesaidiwa na Jado Fidifosi makao makuu yake yakiwa ni Eneo la Vingunguti Kiembe Mbuzi, ambapo Ukumbi wake wa Nyumbani ukiwa ni Mashujaa Pub uliopo katikati ya Vingunguti.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Mamaa Sakina (Cash Lady), amewapongeza kutokana na mwenendo mzuri wa sanaa yao ambayo anasema wakiendelea hivyo wataweza kufika mbali ikiwa ni pamoja na kujipatia kipato na kuweza kujitangaza wao wenyewe kimuziki.

“Ni kinyume na matarajio yetu kwani hatukutarajia kama wasanii hawa wanauwezo mkubwa kiasi hiki ambapo kama unavyosikia tangu waunde kundi hili la Mashujaa pamoja na kwamba ni muda mfupi lakini kazi zao zimeendelea kuonekana ikiwa ni pamoja na kusikiwa katika vituo mbalimbali vya Radio, na kazi zao zimeonekana ni wabunifu wazuri wa masuala ya muziki,”alisema Mamaa Sakina.

Aidha amewasifu kwa utulivu walioonyesha tangu walipoweza kujiunga na kampuni hiyo kwa lengo la kufanya kazi wakiwa kama wanamuziki, ambapo mpaka sasa tayari wameshafanikiwa kurekodi nyimbo mbili ambazo ni Moshi wa Sigara na Mwanike huku wakiwa Studio kukamilisha Wimbo wa Safari yenye Vikwazo unaoonekana kuja kutikisa Dunia kutokana na jinsi wimbo huo ulivyobeba hisia nyingi.

Mmoja wa wanenguaji wake, Mariam Leila pee ambaye kwa sasa ndiye mnenguaji mahiri, anazungumzia historia yake kwamba alitokea Tamaling iliyokuwa Zanzibar kabla ya kuibukia Acudo Impact, Diamond Musica, Vijana Classic kwa sasa anapigiga kazi yake na mashabiki wameikubali mashujaa Musica, na anawambiwa wapenzi wake anaipenda mashujaa kutokana naanakubali kazi ya mashujaa ni ya kimataifa siyo ya kitaifa,

“Mkae mkao wa kula kuangalia kazi ya mashujaa na wanenguaji wa mashujaa na kusikiliza muziki wa ukweli na magitaa ya ukweli kutoka kwa Kiongozi wa kundi Elyston Angai, hatuna mpinzani sisi ni mwanzo na mwisho, tunawapenda sana wapenzi wetu, na mimi kama Leila Pee sijawahi kuona mziki kama mashujaa Big Up Elyston Angai, Jado Fidifosi, Baba Isayan (Chochea), ambao mnafanya kazi kubwa viongozi wangu bendi ya mashujaa Intertainment- Mamaa Sakina, Papaa Maisha, Papaa Yohana, tuko tayari kufanya kazi kwa moyo mmoja hapa kazi tuu Kolala Tee” anasema Leila Pee.

Ni mzaliwa pekee yake kutoka kwa mama Fatma-mkazi wa Dar es Salaam yeye akiwa ni mtoto wa kwanza na mwisho kuzaliwa katika familia yake, ikiwa a maana ni mzaliwa pekee katika tumbo la Fatma mwaka 1984 mwezi wa sita katika hospitali ya Amana jiji Dar es Salaam.

Akizungungumzia historia yake Leila Pee anasema alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kijichi iliyoko katika Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es Salaam alianza kuipenda fani ya muziki tangu akiwa mdogo, alipokuwa akisikia nyimbo za wanamuziki Gato wa nchini Congo, aliyeimba (hazarakise hawaa,) Mwanamuziki Madilu System(Mamuu) ndipo alianza kama mchezo, wakati huo alianza kucheza kwa watu, zinapopigwa nyimbo hizo, na zaidi anasema anakumbuka jinsi Dogodogo Rashidi alivyoweza kumsaidia kipindi hicho kuhusu kazi yake mpaka hatua aliyofikia.

Kwa upande wa Salha yeye ni mzaliwa wa tisa wa familia ya Mzee Salehe Athumani -mkazi wa Kipawa yeye akiwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa (kitinda mimba) katika tumbo la Zainabu Ibrahim mama mzazi wa Salha miaka 23 iliyopita tangu kuzaliwa kwake mwaka 1987 kwenye hospitali ya Amana iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akiwa ni mtoto wa kike wa sita tangu wenzake kutoka tumboni mwa mama yao kuzaliwa, kabla ya kupendwa na mwenyezi Mungu (aziweke roho zao mahali pema peponi-akina Mariam Salehe, Zulfa Salehe, Sophia Salehe, na Amina Salehe), Salha anasema kuwa ndugu zake hao baada ya kufariki, alibaki mpweke kitendo kilichomfanya pia ashindwe kuendelea na masomo kutokana na familia yake kutokuwa na uwezo.

Kwa sasa Salha anasema wamebaki watoto watano wa kike wakiwa ni wawili yeye ya Idayab Sarehe, pamoja na kaka zao Jafari Sarehe, Isiaka Sarehe, na Abubakari Sarehe ambao mpaka sasa wapo wakiendelea kuishi nyumba ya Familia yaani ya Mzee Sarehe Athumani .

Akizungungumzia historia yake Salha Salehe anasema kuwa, alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Kipawa ambayo ipo katika wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam na alifanikiwa kumaliza shule ya Msingi mwaka 2002 bahati mbaya ama nzuri kwake hakuweza kuendelea na masomo kutokana na kuipenda sana fani ya muziki ambapo moja kwa moja alianza safari yake kuelekea katika suala zima la Muziki.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...