Thursday, April 22, 2010

Juan Antonio Samaranch hatunaye tena


Juan Antonio Samaranch (1920 - 2010)
Dunia na hasa ulimwenguwa michezo umempoteza mtu mashuhuri sana, aliyekuwa raisi wa Kamati ya Olimpiki duniani (I.O.C) bwana Juan Antonio Samaranch, ambaye amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 89.

Bwana Samaranch anakumbukwa kwa kuchukua uongozi wa IOC kutoka kwenye kipindi kigumu cha migomo toka nchi mbalimbali na matatizo ya kifedha kiasi cha kutishia kufilisikakwa shirikisho hilo.

Alipoingia madarakani mwaka 1980, bwana Samaranch alibuni na kufanikisha miradi kadhaa ya kuliingizia fedha katika Shirikisho hilo, kiasi cha kulianya kuwa shirika lenye utajiri wa kibilionea. Alitengeneza faida ya dola za Kimarekani milioni mia mbili na hamsini ($250,000,000) kutoka dola laki mbili tu ($200,000) alizozikuta alipoingia madarakani.
Habari kamili. KWA HABARI ZA KINA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HEBU TEMBELEA hapa

1 comment:

Subi Nukta said...

Shukrani kaka Yahya kwa kuweka posti hii katika blogu na ku-linki kwenye wavuti.com
Ninafurahia ushirikiano huu na ninaomba uendelee.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...