Monday, November 02, 2009

Stendi Kuu Ubungo yakabidhiwa kwa serikali



MAkabidhiano ya uendeshaji Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT) jijini Dar es Salaam yamefanyika usiku wa manane kuamkia jana ambapo kampuni inayomilikiwa na familia ya Kingunge ilimaliza mkataba wake rasmi na kukabidhi kituo hicho mikononi mwa Serikali.
Huku akikanusha kuwa kampuni ya Smart Holdings Limited iliyoendesha kituo hicho kuhusika na familia ya mwanasiasa Kingunge Ngombale Mwiru, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hassan Khan aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kampuni yake imemaliza mkataba wake wa miaka mitano ambapo saa sita usiku wa juzi (Jumamosi) ilikabidhi uendeshaji UBT kwa serikali.
"Makabidhiana hayo yalifanyika usiku wa saa sita kwa sababu ya mkataba wetu ulikuwa unaishia tarehe na siku ya 'wikiendi' (Mwisho wa wiki',"alisema Khan na kufafanua kuwa waliokuwepo kwenye makabidhiano hayo ni Mkurugenzi wa Jiji Alhaji Kingobi, uongozi wa jiji wa wakati huo chini ya Wilfred Mukama na utawala wa UBT. Leo watendaji kutoka halmashauri ya jiji wameonekana wakidunda mzigo pasipo utani, wamechachamaa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...