Tuesday, November 10, 2009
Mitambo ya Dowans yakamatwa
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) kupitia wakala wake wa ukusanyaji madeni sugu kampuni ya Majembe Auction Mart "Vijana wa Kazi" jana walipiga kufuli mali za kampuni ya kufua umeme ya Dowans kutokana na TRA kuidai kampuni hiyo Sh 9,120,611,746 ya kodi zake mbalimbali.
Akizungumza kupitia kituo cha televisheni cha taifa (TBC1) jana, Afisa Masoko wa Kampuni ya Majembe Action Mart, Dixion Kitime alisema hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kampuni hiyo kushindwa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedh kwa muda mrefu.
“Tumekamata mitambo ya Kampuni ya Dowans leo (jana) asubuhi na kuanzia sasa inashikiliwa na kampuni yatu kwa kushindwa kulipa deni lake la muda mrefu,”alisema Kitime.
Kitime alitaja baadhi ya mitambo iliyokamatwa kuwa ni makontena nane ya kuhifadhia mafuta pamoja na mitambo mingine.
Alifafanua kuwa mitambo hiyo imekamatwa ili kuwalazimisha wamiliki wake kulipa gharama za Sh 9 bilioni wanazodaiwa na TRA na kusisitiza kuwa kama hawatafanya hivyo ndani ya siku 10 kuanzia leo mali hizo na mitambo itapigwa mnada hadharani. Habari imeandikwa na Geofrey Nyang'oro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment