Thursday, November 12, 2009

Elizabeth wa BBA awasili na kuzungumza


Mshiriki wa Big Brother E,izabeth Gupta akiongea na wanahabari leo hoteli ya Paradise jijini Dar. Kulia ni bosi wa operesheni wa MultiChoice Baraka Shelukindo na shoto ni afisa operesheni wa MultiChoice Grace Urassa. Pamoja na mambo mengine Elizabeth amewashukuru wadau kwa kumpigia kura na kumpa taffu katika kipindi chote alichokuwa mjengoni.

Kasema ana mpango wa kurudi masomoni kwani ndio kwanza kamaliza kidato cha sita hivyo ana kiu ya kusoma sanaa na kuigiza pamoja. amesema anapenda kuigiza na kuimba na ameshawahi kuwa mtangazaji. amesema anatafuta sponsa kujiendeleza katika sanaa na akimkosa atajilipia mwenyewe.



Mshiriki wa Bigbrother Africa Revolution Elizabeth Gupta aliyewasili jana uwanja wa ndege wa mwalimu J.K.Nyerere akitokea sauzi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...