Wednesday, November 11, 2009
Jina la Waziri Msolla latumika kutapeli
Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Peter Msolla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Msolla alikuwa akitoa taarifa juu ya matapeli wanaopigia watu simu kwa watu na kujigeuza sauti zao kufanana na yakwake ili wafanya utapeli wao. Picha na Peres Mwangoka.
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla amesema amedhalilishwa na kuchafuliwa jina lake katika jamii baada matapeli kulitumia jina lake katika kufanya utapeli kwa njia ya simu.
Profesa Msolla aliyasema hayo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusu utapeli kwa njia ya simu kwa kutumia majina ya watu maarufu nchini.
Alisema yeye mwenyewe ameshaathirika na utapeli huo baada ya matapeli hao kutumia jina lake kufanya utapeli huo kwa watu mbalimbali.
Akielezea utapeli huo Profesa Msolla alisema matapeli hao wamekuwa wakiiga sauti yake na kuwapigia watu wakijitambulisha kuwa ni yeye(Msolla) na kwamba ana shida na anaomba kiasi fulani cha pesa.
“Hivi karibuni kumezuka utapeli ambapo watu wanaiga sauti ya mtu na kuzungumza kama ndio mhusika mwenyewe asilia kisha huonesha kuwa ana shida na anahitaji msaada hivyo huomba fedha kutoka kwa watu mbalimbali na kuwaelekeza zitumwe kwenye akaunti za benki mbalimbali hapa nchini;
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
1 comment:
Wananchi,mtu anayetajwa kutapeli kwa kuigiza sauti za watu mbalimbali ni wa siku nyingi,alitaka kumtapeli Naibu Waziri wa Maji Ndg Christopher juzi na mwaka jana alinusurka kukamatwa baada ya kutaka kumwingiza mkenge MD wa DDCA akigiiza sauti ya Chiiza.Kuweni makini na namba anayotumia ndo hiyo hiyo ambayo imeandikwa pia katika gazeti la Mwananchi la tarehe 12/11.Mdau
Post a Comment