Wednesday, September 10, 2008

Mtoto akatwa uume wote akitahiriwa



MTOTO Franciss Gasper, mwenye umri wa mwaka mmoja na mwezi
mmoja (pichani) anakojoa kwa kutumia mpira maalumu baada ya kukatwa uume wake wakati akitahiriwa kwenye zahanati inayofahamika kwajina la Olorein iliyopo Mererani mkoani Manyara.
Mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Spola Onero, 24, aliiambia Mwananchi kuwa alimpeleka mtoto wake katika hospitali hiyo Juni 15 mwaka 2008 kwa nia ya kumtahiriwa na alimkuta dakrati aliyemtaja kwa jina la Elisha Elunde na kumfahamisha kuwa anaweza
kufanya kazi hiyo.
Aliendelea kusema kuwa kabla ya hapo mwanae alikua
akisumbuliwa na maradhi (lawalawa) na kuona umuhimu wa kumtahiri ili kuondokana na maradhi hayo. Lakini baada ya kumtahiriwa mtoto huyo alilia sana na alimrejesha katika zahanati hiyo lakini daktari huyo, alimtoa wasiwasi na kumwambia kuwa uume wa motto wake utarejea taratibu.
"Nilimrudisha hospitali na nikamweleza kuwa mtoto hawezi kukojoa na daktari Elunde akanimbia kuwa nirudi nyummbani na nisimwambie mtu
mpaka mtoto atakapopona. Lakini nikaona mtoto anazidi kulia na uume
hakuna," alisema Bi. Spola kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa mara kwa mara alipomrudisha mtoto kwa
daktari huyo alimwambia kuwa anaomba iwe siri na anafanya jitihada za kumpa dawa ili uume wa mtoto urejee katika hali ya kawaida.
Naye baba mkubwa wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Ray Maseli alisema kuwa aligundua kuwa daktari huyo hakuwa na uwezo wa kumtahiri mtoto huyo baada ya kufanya uchunguzi na hivyo wakaripoti suala hilo kituo cha polisi Mererani na daktari huyo kukamatwa.
Aliongeza kuwa daktari huyo pamoja na kukamtwa aliachiwa huru
siku chache baadaye na kesi haikufunguliwa.
"Tulirejea kituo cha polisi kutoa taarifa upya na ndipo siku ya Alhamisi alikamatwa tena na kupelekwa katika kituo cha polisi kilichopo wilayani Babati. Habari na Hemed Kivuyo, Arusha.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...