Thursday, April 24, 2008
Waliofanya vurugu Chuo Kikuu Dar watimuliwa
Na Waandishi wa Mwananchi
SERIKALI imetangaza kuwafutia udahili na kuwafukuza masomo wanafunzi waliofanya vurugu katika huo Kikuu cha Dar es Salaam.
Taarifa ya serikali iliyosomwa bungeni jana vioni mjini hapa na Waziri wa Elimu na na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ilieleza kwa kifupi kuwa wanafunzi hao wapatao 39 na wengine 300 walioshiriki maandamano wa chuo hicho wamefutiwa udahili na hawataruhusiwa kujiunga na chuo chochote nchini.
“Waliofanya vujo leo (jana) wamefutiwa udahili na kufukuzwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hawataruhusiwa kujiunga na chuo chochote,” alisema Profesa Maghembe katika taarifa hiyo bungeni saa 11.30.
Profesa Maghembe alisisitiza msimamo wa serikali kuwa haitawavumilia watu wanaofanya uhalifu na vurugu badala ya kusoma.
Adhabu hiyo imewakumba wanafunzi 39 waliodaiwa kuwa vinara mgomo ulianza Jamatatu wiki hii ili kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwarudisha chuoni wenzao 15 waliofukuzwa awali kwa tuhuma kama hizo.
Mgomo huo ulifuatwa na vurugu zilizozuka juzi chuoni na kusababisha uongozi wa chuo kutoa taarifa polisi ambao waliwadhibiti wanafunzi hao na kuwakamata baadhi yao huku wengine wakiumizwa vibaya kwenye mapambano hayo. Pichani wanafunzi wa Chuo Kikuu wakigangamala wakitaka wenzao warejeshwe. Picha ya mdau Faraja Jube.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment