Friday, April 11, 2008

mkataba wa TICTS wa kifisadi



Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabuza Serikari, Ludovick Utouh akitoka nje ya ukumbi
wa bunge Dodoma mara baada ya ripoti za hesabu za serikari za mitaa na hesabu za
serikari kuu za mwaka ulioishia tarehe 30 june 2007 kuwasilishwa jana bungeni. Picha
na Edwin Mjwahuzi.

Na Ramadhan Semtawa aliyepo Dodoma

RIPOTI ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali hadi Juni 2007 imetoka kwa kuanisha ufisadi katika ofisi mbalimbali za umma, na kuonyesha mkataba mpya kati ya Kampuni ya Kupakua Shehena za Kontena Bandarini (TICTS) na Mamlaka ya Bandari (TPA), haukufuata taratibu za kisheria.

Hatua ya mkabata huo wa TICTS kuhusishwa na ufisadi ndani ya Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye kisheria ndiye mkaguzi wa hesabu za umma, kunazidi kuthibitisha taarifa za siku nyingi kwamba, mchakato mzima wa kuongezea mkataba wa awamu ya pili kwa Kampuni hiyo umetawaliwa na ufisadi kutokana na kutofuata taratibu za zabuni.

Akisoma ripoti hiyo mjini hapa jana CAG, Ludovick Utouh, alisema maoni ya ofisi ni kwamba hatua ya kuongeza mkataba kwa TICTS kabla ya kumalizika wa awali imekiuka taratibu za Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004, ambayo inahuisisha pia zabuni. Kwa taarifa zaidi soma Mwananchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...