Thursday, April 17, 2008

Bilionea Chenge ndani ya Dar


Akiondoka n akurejea VIP baada ya kumalizana na waandishi.


Baadae huyoo akatimua zake kuendelea na mpambano wa shutuma hizo zilizosisimua watu nchini. Picha hizi ni za mdau Mpoki Bukuku.

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge amerejea nchini jana akitokea China na kusema kuwa mambo yote anaachia vyombo vya uchunguzi ili kuthibitisha tuhuma za rushwa dhidi yake.

Alisema katika Uwanja wa ndege wa Dare s Salaam leo alasiri kuwa akiwa mwanasheria hawezi kuzungumzia shutuma ambazo bado ziko katika hatua ya uchunguzi.

"Unapotuhumiwa, uchunguzi unafanyika, kwa kanuni na taratibu za uchunguzi, siruhusiwi kuzungumza. Kwa sasa ni mapema mno, tuvipe nafasi vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake,"

"Hoja ya msingi hapa ni kwamba, nimelipwa fedha na Kampuni ya BAE System (ya Uingereza) katika ununuzi wa rada. Tuhuma hiyo ni nzito kweli kweli na siyo ya kuropoka,"

“wakimaliza uchunguzi wao then wakuliza Bw. Chenge hivi vijisenti ulivipateje ndipo ntaeleza,”

Tuhuma dhidi ya Chenge za kujilimbikizia fedha hizo, ziliibuliwa na gazeti la The Guardian la Uingereza, ambalo lilieleza kuanza kwa uchunguzi dhidi ya waziri huyo baada ya wachunguzi kukuta na zaidi ya dola za Marekani milioni moja (sh bilioni moja za kibongo).

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai nchini humo ya Serious Fraud Office (SFO), inatarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo, ili kuangalia iwapo zina uhusiano wowote na zile zinazoaminika kutolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi za Uingereza milioni 28, ambazo ni sawa na Sh 70 bilioni, mwaka 2002.

No comments: