Sunday, April 06, 2008

Serikali yawapigia magoti wafanyakazi TRL

* Yaikopesha zaidi ya Sh3.6 bn kuongeza mishahara
* Wafanyakazi sasa kulipwa mishahara mipya





HATIMAYE Serikali imeingilia kati mgomo wa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), uliosababisha kusitishwa kwa huduma za usafirishaji wa reli ya kati baada ya kuikopesha kampuni hiyo kiasi cha Sh 3.6 bilioni kwa ajili ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi wake.

Uamuzi huo wa serikali, umewafurahisha wafanyakazi hao na kutangaza kusitisha mgomo wao mara moja na kurudi kazini baada ya madai yao ya kutaka kulipwa mshahara wa Sh 160,000 kwa kima cha chini kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumza na wafanyakazi hao kwenye makao makuu ya kituo cha reli cha kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema serikali imelikopesha zaidi ya Sh3.6 bilioni ili liweze kuwalipa wafanyakazi hao mishahara hiyo mipya kwa kipindi cha miezi mitano.

2 comments:

Anonymous said...

Samahani nipo nje ya topiki kidogo.Tatizo lenu hizi blogs za wabongo mnakopiana kila kitu.Kama hizi picha nimeziona zote kule kwa Haki Ngowi.Sasa nani kamchukulia mwenzake picha?Muwe basi mnatoa attribute wanawane.Na kama mmoja kamuibia mwenzake basi sio mnachukuliana zoooote!Wasomaji wenu tunataka vitu vipya na tofauti tofauti..ndio maana ya blogs.

Anonymous said...

WEE KIBUYU, MAAANA YA BLOG UNAYOJUA WEWE NI YA KWAKO EBO, MBONA HUSEMA KULE KWA MJENGWA,BONGOCELEBRITY WANASHIRIKIANA KUCHUKUA PICHA KWA WANA BLOG WENZAO,HUYU CHARAHANI NIMEONA MIMI MARA SI MOJA AKIMTAJA HUYO HAKI NGOWI,INAWEZEKANA NI WATU WA KARIBU.SISI SI KAZI YETU
INAONEKANA WEWE UNA KISIRANI CHAKO BINAFSI,EBWANA CHARAHANI KAMUA BABA HATA UKWIEZA NENDA KWENYE WEBSITE NYINGINE MWAGA HABARI HUKU SISI TUTAENDELA KUPITA BILA WASI WASI,KUMBUKENI USHIRIKIANA WA WANA BLOG NDIO MUHIMU KWETU WE KAMA UNATAKA VITU VIPYAA ANZISHA YA KWAKO KIBOGO WE..
MDAU
KL

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...