Friday, April 25, 2008
Akudo Impact
Muziki wa dansi hapa nchini hivi sasa umeonekana kuvaa sura mpya kutokana na kupendwa zaidi na watu tofauti na awali. Kumekuwa na bendi kadhaa hapa nchini ambazo zimekuwa zikivuma sana huku zikijipatia mashabiki lukuki.
Bendi hiyo hivi sasa inaitwa Akudo Impact ambayo ina muda wa mwaka mmoja lakini imeweza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na vipaji vilivyo jaa katika bendi hiyo.
Bendi inaongozwa na Taksis Masela ambaye ni makamu kiongozi mkuu aliyewahi kuimba katika bendi ya Felix Wazekwa anasema bendi ina jumla ya wanamuziki 19. pia wapo Taxis Masela Jqoto ambaye nilikuwa BCBG, Zegre Butamu ambaye alikuwa BCBG, Alan Kabasele ambaye alikuwa Empire Bakuba ( ya Lofombo) nao waliungana kuunda Akudo. Nwijac alimkuta kwa Fere gola, Canal Top aliyekuwa kwenye bendi ya Wenge BCBG ya JB Mpiana,
Yupo mpiga gitaa la solo Mechant imbwa mukali kutoka katika bendi ya Wenge El Paris , De Kanto mpiga gitaa la bass kutoka Extra Muzika. Buffalo Maziwi aliyetokea BCBG ambaye anapiga ngoma".
Wanenguaji wake ni kiboko wacheki Nasi ambaye alikuwa mnenguaji kutoka katika bendi ya Koffie Olomide, Shushuu nae kutoka kwa Coffie na Faally. Josline aliyetoka kwa Empire Bakuba ya Djuna Mumbafu, Karen kwa Redy Amis.
Kiongozi mukulu kabisa ni Christian Bella maarufu kama 'Tajiri ya Masauti'' Bendi hiyo hivi sasa inajiandaa na uzinduzi wa albamu yake ya kwanza. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 16 mwaka huu, katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Hebu pata burudani hii kutoka Harieth Makweta wa Mwananchi usome kwa kina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment