Sunday, March 22, 2026

MSIGWA: SERIKALI IMEWEKEZA ZAIDI YA TRILIONI 1 USAFIRI WA MAJINI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg, Gerson Msigwa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkoa wa Mwanza, leo Machi 22, 2026, katika Bandari ya Mwanza South, jijini Mwanza

Na. Fullshangwe Blog, Mwanza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza miradi ya usafiri na usafirishaji majini yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni moja katika maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa pamoja na Bahari ya Hindi.

Amesema kuwa meli ya MV Mwanza ni moja ya mafanikio makubwa ambapo ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 400, na ni miongoni mwa meli kubwa zaidi katika maji baridi barani Afrika.

Aidha, amebainisha kuwa ujenzi wa meli hiyo umegharimu shilingi bilioni 123 na ulikuwa umefikia asilimia 40 wakati Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani mwaka 2021, lakini sasa umekamilika kwa asilimia 100.

Pia ameongeza kuwa vijana takribani 200 wakiwemo mainjinia na mafundi walipata ujuzi kwa kushirikiana na wakandarasi kutoka Korea katika ujenzi wa meli hiyo.

No comments:

SAMIA AZINDUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WFNS, ATEMBELEA MAONESHO YA SEKTA YA AFYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitembelea mabanda ya maonesho ya wadau wa Sekta ya Afya kabla ya k...