Sunday, August 02, 2026

TAWIRI YASHIRIKI MKUTANO WA KIMKAKATI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII





Mkurugenzi Mkuu TAWIRI Dkt. Eblate Mjingo ni miongoni mwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wanaoshiriki  mkutano wa  kimkakati unaowajumuisha  watendaji wote wa Wizara hiyo kujadili  namna bora ya kuboresha utendaji ili kufikia malengo tarajiwa hususani ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.

Akifungua mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameitaka Menejimenti ya Wizara na Wakuu wa Taasisi za Wizara hiyo  kuongeza ubunifu sambamba na  kuzigeuza  changamoto za kiutendaji kuwa fursa za matokeo chanya kwa wananchi.

Amefafanua kuwa sekta ya Maliasili na Utalii ni moja ya sekta za mageuzi hapa nchini kutokana na mchango wake katika kuchochea ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira, mapato ya fedha za kigeni na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

“ Utendaji katika sekta hii  ni lazima uwe wa kimkakati na unaozingatia utu kwa kuwa unagusa sehemu kubwa ya maisha ya wananchi,” amehimiza Dkt. Kijaji

Mkutano huo unaoendelea kwa siku nne katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere ni fursa kwa Menejimenti na viongozi wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu bora za kuendeleza uhifadhi na utalii.

TAWIRI ni injini katika sekta ya Uhifadhi na Utalii

No comments:

MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI AWASILI VIENNA, TANZANIA YAINGIA JUKWAANI KUJADILI NGUVU YA ATOMU KWA MAENDELEO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi akiongoza kikao cha Maandalizi cha Viongozi na Wataalamu mbali...