Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tayari amewasili
katika Ukumbi wa Chandamali Songea kwa ajili ya Mdahalo wa Kitaifa wa
Maadili leo Septemba 14, 2024, ikiwa ni kuelekea Tamasha la tatu la
Utamaduni la Kitaifa kuanzia Septemba 20 hadi 23, 2024 Uwanja wa
Majimaji Songea.
Mhe. Waziri akiwa ameambatana na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma amepokelewa na baadhi Viongozi wa Wizara na Taasisi zake.
Mdahalo huo utahusisha mada mbalimbali zitakazojadiliwa, makundi ya wazee, vijana pamoja na wanachuo.
No comments:
Post a Comment