TAIFA STARS YANG’ARA GUINEA




Tanzania imepata ushindi wa muhimu katika harakati za kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Guinea. 

Katika mechi hiyo iliyochezwa katika Houphet Boigny, Ivory Coast wachezaji kutoka Tanzania walionyesha kiwango cha hali ya juu kwa kufunga mabao mawili yaliyowapa Stars alama tatu muhimu.

Katika mchezo huo, Feisal Salum Zanzibar Finest alifunga goli la kwanza kwa mkwaju mkali kwa upande wa Tanzania, huku Mudathir Yahya Zanzibar Greatest akiongeza goli la pili. Mabao haya yamesaidia Tanzania kufikisha jumla ya alama 4 katika kundi lao, hali inayoimarisha nafasi yao katika mbio za kufuzu kwa AFCON 2025.

Guinea walitangulia kupachika goli la mapema ambalo walibakia nalo, lakini haikuwa ya kutosha kuweza kuzuia ushindi wa Tanzania. Ushindi huu unakuja kama faraja kubwa kwa timu ya taifa na mashabiki wake, na umeongeza matumaini ya kufuzu kwa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Comments