Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya hati miliki na kibali cha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya kanda ya mamlaka hiyo hafla hiyo imefanyika leo.
Baadhi ya wadau, washiriki na Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa na wale wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira wa Arusha (AUWSA) wakifuatilia makabidhiano hayo ya hati miliki na kibali cha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya kanda ya mamlaka hiyo hafla hiyo imefanyika leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi hati miliki Mhandisi Humphrey Mwiyombela, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA), wakati wa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi hati miliki Mhandisi Humphrey Mwiyombela, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA), wakati wa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani ambaye pia alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi hati miliki Mhandisi Humphrey Mwiyombela, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA), wakati wa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Banyani kwenye makabidhiano hayo ya hati miliki na kibali cha ujenzi wa Jengo la makao makuu ya kanda ya mamlaka hiyo hafla hiyo imefanyika leo.
HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA, DK. MAULID
BANYANI KWENYE MAKABIDHIANO YA HATI YA KIWANJA
NAMBA 926, KITALU ”B”, BURKA MATEVES CHA UJENZI WA MAKAO MAKUU KWA MAMLAKA YA
MAJI SAFI NA MAJI TAKA ARUSHA (AUWSA), TAREHE 15 NOVEMBA 2018
Ndugu Richard Kwitega, Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,
Mhandisi Dk. Richard Masika, Mwenyekiti wa Bodi wa
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA),
Mhandisi Humphrey Mwiyombela, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA),
Afisa Ardhi wa Jiji la Arusha, Dickley Nyato ambaye ni
mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji,
Mwakilishi kutoka TARURA,
Mwakilish wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa,
Mwakilishi kutoka Zimamoto,
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mlongoine
Wakurugenzi na Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa
Wadau wetu katika uendelezaji wa Kitovu chetu cha mji wa Safari City
Ndugu Wageni Waalikwa,
Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana, itifaki imezingatiwa.
Awali ya yote namshukuru
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma kwa kutuwezesha kukusanyika pamoja wakati huu
hapa katika tukio hili muhimu la makabidhiano ya hati ya kiwanja kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), tukio hili
limetanguliwa na makabidhiano ya kibali cha ujenzi asubuhi hii.
Pia nachukua fursa hii
kuwashukuru waandaaji wa hafla hii kwa kuiandaa vyema kwani upo usemi usemao shughuli ni watu na watu ndiyo sisi
imependeza, niwashukuru pia kwa kunialika kushiriki nanyi katika makabidhiano haya.
Nichukue fursa hii pia kuwakaribisha wadau wetu kutoka Jeshi la Polisi,
Zimamoto na Wateja wetu wa hapa Safari City.
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana
Hii ni mara yangu ya kwanza
nafika hapa Matevez tangu niteuliwe kushika wadhifa huu na nimefarijika sana kuona
hatua kubwa zinazoendelea kupigwa kila uchao katika utekelezaji wa mradi huu, tusilale
tuhakikishe tunafanya kazi kwa bidii na tija huku tukitimiza malengo ya nchi
kuweza kuwajengea wananchi nyumba bora na pia kuwapangia makazi makazi katika
vitovu vya miji kama hivi. Nawaahidi kuendeleza jitihada hizo na nitafanya kazi
kwa bidii kwa manufaa ya Watanzania wote.
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana
Kama mnavyofahamu mradi huu wa kitovu cha mji wa
kisasa wa SafariCity wenye ukubwa wa ekari 587.5 ni sehemu ya mji
iliyopangiliwa kitaalamu na kwa kuzingatia sheria za mipango miji. Mradi huu
ulibuniwa na Shirika kwa lengo la kupunguza tatizo la msongamano katikati ya
Jiji la Arusha na kupunguza uhaba wa makazi kwenye Jiji hili.
Jukumu mojawapo la Shirika la Nyumba la Taifa ni
kuwa Mwendelezaji Mkuu wa Miliki nchini ambapo lina Mamlaka ya kupanga miji,
kuisimamia na kuhamasisha uendelezwaji wake. Shirika, wananchi pamoja na
taasisi mbalimbali zimeshiriki katika uendelezaji wa pamoja wa kitovu hiki cha
Mji cha mfano, ambacho ni cha kwanza kuendelezwa hapa nchini katika mfumo huu.
Katika muktadha huo, Shirika
liliingia makubaliano rasmi na AUWSA, baada ya Mamlaka hiyo kuomba kupatiwa
eneo katika la mradi wa SafariCity kwa malengo mahususi ya kujenga ofisi kuu ya
kanda ya mkoa wa Arusha kwa shughuli za kiofisi pamoja na kuhakikisha huduma
bora za maji zinapatikana kwa wakazi wa jiji la Arusha.
Awali, katika mpango
kabambe wa kuendeleza mji wa SafariCity, Shirika liliweka mkakati wa vipaumbele
vya miundombinu mbalimbali ili kuhakikisha wanunuzi wa viwanja pamoja na nyumba
wanapata na kuitumia kwa uhakika miundombinu hiyo pasipo kupata shida yeyote.
Miundombinu hiyo ni pamoja na barabara, maji na umeme.
Ili kuhakikisha huduma ya
maji inapatikana, Shirika liliingia gharama za kuleta maji katika mji wa SafariCity
kwa lengo la kuwezesha wateja walionunua nyumba na viwanja wanapata maji ya
uhakika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shughuli mbalimbali zinazohitaji huduma
za maji katika mji wa SafariCity zinaendelea vizuri. Shughuli hizo ni ujenzi na
umwagiliaji wa miti iliyopandwa na Shirika katika viwanja vyote vilivyofunguliwa
kwa ajili ya mauzo.
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana
Katika moja ya makubaliano
hayo, Shirika lilikuwa na jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa hati kwa Mamlaka
ya Maji. Jukumu hilo limefanikiwa na hivi leo Shirika linayo furaha kukabidhi
rasmi hati miliki hiyo kwa Mamlaka kwaajili ya kuhakikisha ujenzi wa Ofisi kuu
unaanza. Nimedokezwa hapa kwamba Mamlaka ya AWSA hawajabaki nyuma kwani
walishaweka mkandarasi eneo la ujenzi, ni furaha yetu kwamba watahakikisha
miundombinu ya Maji inaendelezwa kama ilivyokusudiwa.
Mpaka sasa tuna wanunuzi
130 ambao tayari wamepatiwa hati miliki zao. Hivyo basi tunawategemea
kuendeleza viwanja vyao mara tu Mamlaka ya Maji itakapoanza kuambaza maji,
niwahimize tu wautumie muda waliopewa na mamlaka kuendeleza maeneo yao ili muda
usije kuwapita. Hiyo itapelekea SafariCity kuwa na muonekano wake halisi kama
inavyotazamiwa na Shirika, wananchi na Serikali kwa ujumla.
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana
Mwisho kabisa, Shirika la
Nyumba la Taifa linategemea kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Mamlaka ya
Maji katika kuhakikisha miundombinu ya maji inakamilika kwa wakati katika mji
wa SafariCity. Pia tunategemea sasa iwe chachu kwa wanunuzi wote wa viwanja
kuanza ujenzi wa nyumba zao ili kutimiza malengo ya Shirika na Serikali kwa
ujumla.
Aidha, Shirika linaendelea
kushirikiana na taasisi mbalimbali za Kiserikali zenye dhamana ya kuhakikisha
miundombinu salama inaendelea kuendelezwa katika mji wa SafariCity, zikiwemo TANESCO upande wa
miundombinu ya umeme, pamoja na TARURA (Wakala wa huduma za barabara mijini na
vijijini) kwa upande wa miundombinu ya Barabara. Pia polisi na kikosi cha
zimamoto ambao tayari Shirika limeshawapatia viwanja katika mji wa SafariCity.
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
No comments:
Post a Comment