Friday, November 30, 2018

WAFANYAKAZI NHC WAHITIMU NA KUTUNUKIWA SHAHADA ZA UZAMILI

 Wafanyakazi waandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa wamehitimu shahada zao za Uzamili za Kozi mbalimbali za Chuo Kikuu cha Mzumbe ambapo Veronica Mtemi ametunukiwa Shahada ya Uzamili ya Utawala (Master in Public Administration), Michael Chilongani ametunukiwa Master in Procurement and Supply Chain Management na Ritha Mokimirya ametunukiwa Master of Business Administration in Corporate Management.
 Subira Nkato ametunukiwa Master of Business Administration in Corporate Management katika mahafali ya 17 ya Chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, yaliyofanyika tarehe 30 Novemba 2018, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Convention Centre
Veronica Mtemi ametunukiwa Shahada ya Uzamili ya Utawala (Master in Public Administration), Michael Chilongani ametunukiwa Master in Procurement and Supply Chain Management na Ritha Mokimirya ametunukiwa Master of Business Administration in Corporate Management.
Mkadiriaji Majenzi Benedictor Wazaelly ametunukiwa shahada ya uzamili ya Sayansi ya Chuo cha IFM ya MSc in Finance and Investment.

Thursday, November 29, 2018

UONGOZI WA CRDB WATEMBELEA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA, WAJADILIANA MASUALA MBALIMBALI

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani  akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela ambaye alifika makao makuu ya NHC na Watendaji wake wakuu kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu ujenzi wa makao makuu mapya ya Benki ya CRDB yanayojengwa na NHC eneo la Palm Beach. Wakurugenzi hao kwa pamoja wameeleza kufurahishwa na michakato na mahusiano ya taasisi hizo mbili kubwa nchini kwenda vizuri.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani  akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani  akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela.

Jengo la Makao Makuu mapya ya Benki ya CRDB yanayojengwa na NHC eneo la Palm Beach linavyoonekana kwa sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela akitia saini kitabu cha wageni huku Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani akishuhudia na Watendaji wakuu wa NHC na CRDB. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani   akimkaribisha Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka wakati uongozi wa CRDB ulipofika NHC kujadiliana masuala mbalimbali ya kiushirikiano.

Mkutano baina ya viongozi wakuu waandamizi wa benki ya CRDB na wale wa NHC ukiendelea kwenye makao makuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Kambarage House

 Mkutano baina ya viongozi wakuu waandamizi wa benki ya CRDB na wale wa NHC ukiendelea kwenye makao makuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Kambarage House
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela akifafanua jambo kwenye mkutano huo huku Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani akifuatilia. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela akifafanua jambo kwenye mkutano huo huku Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani akifuatilia. Picha ya pamoja baada ya Mkutano baina ya viongozi wakuu waandamizi wa benki ya CRDB na wale wa NHC ukiendelea kwenye makao makuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Kambarage House. 
  Picha ya pamoja baada ya Mkutano baina ya viongozi wakuu waandamizi wa benki ya CRDB na wale wa NHC ukiendelea kwenye makao makuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) , Kambarage House

Wednesday, November 28, 2018

UTARATIBU WA MALIPO KUPITIA GEPG

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LACHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI KISARAWE

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akielezea sifa za eneo la Vigungu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani wakati msafara huo wa Mkurugenzi Mkuu ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko. Eneo hilo liko katika Barabara kuu iendayo Kibaha na eneo limetenganishwa na viwanda kwa barabara hiyo iendayo Kibaha. Matangi mawili ya kuhifadhia maji, yenye uwezo wa lita milioni tano, yatajengwa katika maeneo ya karibu na hapo, kwa ajili ya viwanda na makazi mapya; na Minarani kwa ajili ya mji wa Kisarawe kwa gharama ya Sh bilioni 10.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani akitia saini kwenye kitabu cha wageni cha Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alipotembelea ofisi hizo kabla ya kutembelea baadhi ya fursa za uwekezaji  wilayani Kisarawe ambapo Shirika la Nyumba la Taifa linaweza kushirikiana na Wilaya hiyo katika uwekezaji maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na eneo la  Community Hall,  Stendi ya zamani na eneo kunakotarajiwa kuanza kupimwa viwanja vya makazi na shughuli mchanganyiko la Vigungu lililopo nje kidogo ya mji wa Kisarawe. 

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa, ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani. 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba akiukaribisha ujumbe kutoka NHC na kisha kuwatambulisha maafisa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. 

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kuelekea eneo la  Community Hall lililopo jirani kabisa na zilipo Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo walipotembelea eneo la Stendi ya zamani Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani leo.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo walipotembelea eneo la Stendi ya zamani Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani leo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba akielekeza jambo msafara huo ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko eneo hilo liko katika Barabara kuu iendayo Kibaha na eneo limetenganishwa na viwanda kwa barabara hiyo iendayo Kibaha. Matangi mawili ya kuhifadhia maji, yenye uwezo wa lita milioni tano, yatajengwa katika maeneo ya hayo, kwa ajili ya viwandana makazi mapya; na Minarani kwa ajili ya mji wa Kisarawe kwa gharama ya Sh bilioni 10.

Eneo la  Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko eneo hilo liko katika Barabara kuu iendayo Kibaha na eneo limetenganishwa na viwanda kwa barabara hiyo iendayo Kibaha. Matangi mawili ya kuhifadhia maji, yenye uwezo wa lita milioni tano, yatajengwa katika maeneo yaVigungu, kwa ajili ya viwandana makazi mapya; na Minaranikwa ajili ya mji wa Kisarawe kwagharama ya Sh bilioni 10.

Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani na ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwenye eneo la Vigungu wakati msafara huo wa Mkurugenzi Mkuu ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani na ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwenye eneo la Vigungu wakati msafara huo wa Mkurugenzi Mkuu ulipokuwa katika eneo la Vigungu kunakotarajiwa kupimwa kwaajili ya uendelezaji wa makazi na shughuli mchanganyiko.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akizungumza na ujumbe wa Shirika la Nyumba la Taifa, ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani na ujumbe wake akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo mbele ya ofisi  ya Mkuu wa Wilaya.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Banyani akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo mbele ya ofisi  ya Mkuu wa Wilaya.

Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Monday, November 26, 2018

NHC KUJENGA MAJENGO MATANO YA WIZARA KATI YA 22 ZINAZOJENGWA MJI WA SERIKALI DODOMA

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na wale wa Wizara ya Fedha na Mipango wakikabidhiana eneo kutakakojengwa ofisi za muda za Wizara ya Fedha, katika eneo hilo Serikali inajenga ofisi za muda za Wizara 22 . NHC imepewa kujenga majengo matano ya Wizara. Leo Shirika la Nyumba limekabidhiwa eneo la Wizara ya Fedha na Mipango. Mji huo huo wa Serikali unajengwa eneo la Mtumba katika Kata ya Mtumba, Tarafa ya Kikombo, lina ekari 1,524 sawa na hekta 617 na lipo umbali wa kilometa 30 nje kidogo ya mji wa Dodoma. Mpaka kukamilika kwake ujenzi unatarajia kuchukua miaka 10 na kugharimu Sh trilioni 10.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NC) na wale wa Wizara ya Fedha na Mipango wakikagua eneo kutakakojengwa ofisi za muda za Wizara ya Fedha, katika eneo hilo Serikali inajenga ofisi za muda za Wizara 22 .
Msafara wa magari ya Shirika la Nyumba la Taifa (NC) na wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa makabidhiano ya eneo kutakakojengwa ofisi za muda za Wizara ya Fedha, katika eneo hilo Serikali inajenga ofisi za muda za Wizara 22 .

Picha ya pamoja ya watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NC) na wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa makabidhiano ya eneo kutakakojengwa ofisi za muda za Wizara ya Fedha, katika eneo hilo Serikali inajenga ofisi za muda za Wizara 22 .

Saturday, November 24, 2018

MKURUGENZI MKUU NHC AAGIZA WIKI YA MWISHO YA KILA MWEZI KUWA YA MAZOEZI

 Mazoezi ya viungo yakiendelea baada ya matembezi ya hisani yaliyofanyika kutokea Chuo Kikuu Ardhi mpaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kurudi Chuo Kikuu Ardhi.

Mazoezi ya viungo yakiendelea baada ya matembezi ya hisani yaliyofanyika kutokea Chuo Kikuu Ardhi mpaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kurudi Chuo Kikuu Ardhi.
 Matembezi ya Hisani ya kilomita tano (5) ya Kusanyiko la Waliowahi kuhitimu na wanaokitakia mema Chuo Kikuu cha Ardhi yamefanyika leo (Jumamosi)  matembezi yameanza saa kumi na mbili asubuhi kwenye jengo la utawala la Chuo Kikuu Ardhi hadi Container na Dispensary Chuo kikuu DSM na kurudi ARU Washiriki kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wameshiriki kikamilifu  Mkurugenzi Mkuu Dk. Maulidi Banyani ameagiza kwamba mazoezi na matembezi ya namna hii  sasa yatakuwa ni lazima kila mwezi mara moja na itaitishwa roll call ili kuhakikisha ushiriki na kuimarisha afya za wafanyakazi.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...