Tuesday, April 05, 2016

KAIRUKI ATOA WIKI MOJA KWA WAAJIRI KUWASILISHA WATUMISHI HEWA

ay1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Angelina Kairuki akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mchakato unaoendelea wa kubaini watumishi hewa Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
ay2
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu toka Ofisi ya Rais Utumishi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Angelina Kairuki alipokutana na waandishi wa habari kuelezea mchakato unaoendelea wa kubaini watumishi hewa Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
ay3
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Angelina Kairuki wakati akielezea  mchakato unaoendelea wa kubaini watumishi hewa Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
ay4
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Angelina Kairuki alipokutana na waandishi wa habari kuelezea mchakato unaoendelea wa kubaini watumishi hewa Serikalini, mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Jacquiline Mrisho-MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi Angela Kairuki amewapa wiki moja waajiri wa sekta za umma  nchini kukamilisha na kuwasilisha taarifa kuhusu watumishi hewa.
Bibi Kairuki ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokua akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa za awali juu ya watumishi hewa zilizowasilishwa na Wakuu wa Mikoa nchini.
Hadi sasa taarifa hizo za Mikoa zimebaini  jumla ya watumishi hewa 1830 ambapo idadi hiyo inazidi kuongezeka kadri utafiti unavyondelea kufanyika.
“Tunatumia zaidi ya asilimia 51 ya pato la ndani kwa ajili ya mishahara na stahiki za wafanyakazi wa Serikalini, sasa kama waajiri hawatowataja na kuwasilisha  watumishi hewa tutazidi kupoteza pato la Taifa, Ofisi imewaagiza waajiri wote kuwasilisha taarifa zao wiki hii ili kuiwezesha ofisi hii na Serikali kiujumla ili kujua kwa usahihi watumishi hewa ni wangapi na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na mamlaka hizo za ajira” alisema Bibi Kairuki.
Waziri Kairuki ameongeza kuwabaada ya ukusanyaji wa watumishi hewa kuisha, ofisi yake itafanya ukaguzi kwenye sekta zote za umma nchini ili kuhakikisha watumishi hewa wote wanaondolewa pia waajiri  watakaokua hawajawawasilisha watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha,Bibi Kairuki amesisitiza kuwa jukumu la kuwaondoa watumishi sio la ofisi ya Utumishi bali ni dhamana aliyopewa  mwajiri wa sehemu husika. Hivyo amewataka waajiri kutimiza wajibu wao.
Amewataka waajiri waambatanishe vielelezo vilivyokosekana katika taarifa za awali za watumishi hewa vikiwemo; majina, vyeo vyao, vituo vya kazi, namba zao za utambulisho (Check No) pamoja na sababu za kuwaondoa katika orodha ya malipo.
Hatua hii imefanyika baada ya agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Machi 15 mwaka huu alipokua akiwaapisha Wakuu wa Mikoa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...