Wednesday, April 20, 2016

DENMARK YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MUZIKI KWA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TASUBA)

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa  Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo Leah Kihimbi akizindua mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)  na
Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika
katika Chuo cha Sanaa mjini  Bagamoyo mkoani Pwani jana.
 Msimamizi wa program wa Kituo cha Utamaduni na Maendeleo Denmark (CKU) hapa Nchini,Mandolin Kahindi akielezea utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa
ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba) , Michael Kadindena akitoa neno la shukrani wakati wa
hafla hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo, Leah Kihimbi akipiga kinanda wakati wa uzinduzi wa mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBA)
 na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi
huo ulifanyika katika Chuo cha sanaa Bagamoyo jana. Wanaoshudia katikati ni  
KaimuMtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba)  Michael Kadindena kulia ni Mratibu wa Mradi huo, Melkiades Banyanka.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa  Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Leah Kihimbi akipuliza Tarumbeta ambacho ni moja ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Kituo cha utamaduni na maendeleo cha Denmark (CKU).
 Meza kuu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari
,Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Leah Kihimbi (katikati) akiwa pamoja na viongozi
wengine wakifuatilia burudani kutoka kwa wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)
  wakati wa uzinduzi wa mradi huo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...