Saturday, April 30, 2016

RC PAUL MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA USAFI JIJI LA DAR LEO


Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda akiwahutubia Wananchi mbalimbali mapema leo asubuhi katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar mara baada ya kumaliza kufanya usafi na hatimae kukusanyika kwenye viwanja hivyo,ambapo Mh.Paul Makonda alizindua kampeni ya Usafi kwa jiji la Dar.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke ndugu Bakari Makere,kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa Paul Makonda katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ya Usafi kwa jiji hilo.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Juma Mgendwa. 
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliokuwa yakijiri uwanjani hapo

MAZISHI YA MZEE PIUS MKUNJA YAFANYIKA MKOANI MOROGORO


Mazishi ya Marehemu Mzee Pius Joseph Mkunja (90), aliefariki April 25,2016 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mkoani Mwanza yamefanyika Mkoani Morogoro
….
Marehemu Mzee Pius amezikwa jana nyumbani kwake Mpanga Kilombero. Alifariki kutokana na tatizo la vidonda vya tumbo lililokuwa likimsumbua. Enzi za Uhai wake alikuwa mfanyabiashara maarufu Mkoani Morogoro.
Katikati pichani juu ni Idda Adam ambae ni mmoja wa Watoto wa Marehemu Mzee Pius, akiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika mazishi hayo.
Kaburi la Marehemu Mzee Pius Joseph Mkunja
Wa kwanza kushoto ni Mtoto wa Marehemu Idda Adam akiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika mazishi hayo.
Tunatoa pole kwa wote walioguswa na msiba.
Bonyeza Hapa kutazama Mwili wa Marehemu Ukiagwa Mkoani Mwanza
Ufunguzi wa Hypermarket kubwa kuliko Mwanza unaendelea hivi sasa katika Mall ya Rock City Mwanza.

Hypermarket hii ambayo ni tawi jingine jipya la TSN linatazamiwa kuwahudumia wakazi wa Mwanza waliokuwa wakikosa uhondo wa bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu zikiwemo mbogamboga fresh kutoka hapa hapa nyumbani.

Akizungumza katika ufunguzi huo masaa machache yaliyopita Mkurugenzi wa TSN alisema,Tanzania Sisi Nyumbani  TSN itatoa zawadi kwa watu 100 wa mwanzo kufika katika uzinduzi huo. 

"Hii ni hatua nyingine kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata vitu fresh.. kutoka nyumbani tena kwa bei nafuu.Tanzania Sisi Nyumbani tunahakikisha Watanzania wanafurahia mazao yao wenyewe...tena kwa bei ya gengeni katika Hypermarket hii.. Wateja wetu ni majirani zetu... karibuni sana TSN Hypermarket Mwanza." alisema.
 Sehemu ya mpnagilio wa bidhaa kwa ndani kama zinavyoonekana. 
 Sehemu ya malipo kwa ndani kama inavyoonekana
 Bidhaa ain ya mboga mboga fresh kabisa 
 Bidhaaa mbalimbali zikiwa ndani ya TSN,tayari kwa wateja kuanza 
Watu na wateja mbalimbali wamefika kujionea Hypermarket hiyo ya kisasa kabisa ndani ya jiji la Mwanza.

TPDC yakanusha kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic


Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic.

Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya  ESCROW  ni Akaunti  maalumu inayoweza kufunguliwa  baina ya  Kampuni, Taasisi,  au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu. Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia. 

TPDC ilifungua Akaunti tatu za Esrow baada ya Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili  kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kutoka Benki ya Exim ya China. Mkopeshaji alipendekeza Akaunti hizo zifunguliwe kwenye benki ya Stanbic na ambapo taratibu za manunuzi zilizingatiwa, ikiwemo ushindanishaji wa watoa huduma.

 Akaunti hizo tatu zilizofunguliwa ni pamoja na:
1. Akaunti ya Mapato ya Gesi 
Lengo la akaunti hii ni hifadhi mapato yote yatakayo tokana na mauzo ya gesi kwa njia ya bomba jipya.

2. Akaunti ya Uendeshaji 
Akaunti hii ina jukumu la kuhifadhi fedha zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa mradi wa miundombinu hiyo mipya ya gesi asilia.

3. Akaunti ya Kulipia Deni
Akaunti hii imefunguliwa kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na mkopo.

Akaunti hizi zinadhibitiwa na masharti yaliyowekwa kwenye makubaliano (Mkataba) ya Menejimenti ya Akaunti hizo yaliyosainiwa kati ya Benki ya Stanbic (kama Benki ), TPDC (kama mtumiaji wa mwisho), Benki ya Exim ya China (kama Wakopeshaji) na Wizara ya Fedha (kama mdeni kwa niaba ya Serikali ya Tanzania).

TPDC inapenda kuufahamisha umma kwamba, baada ya taratibu zote hizo kufuatwa, si sahihi kuuhusisha mchakato huu na tuhuma zozote na ukiukwaji wa sheria za nchi. Aidha, ifahamike kwamba Akaunti ya ESCROW ni akaunti ya kawaida kabisa katika utekelezaji wa miradi kama huu wa gesi asilia.

TPDC Kwa Maendeleo ya Taifa!
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji- TPDC
S.L.P 2774
Dar Es Salaam

DAWA NA VIFAA TIBA KUWA NJIANI MIAKA MINNE BOHARI YA DAWA (MSD) YATOA UFAFANUZI

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akionesha moja ya nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka MSD Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako Mwakalobo. 
 Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza na wanahabari.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Terry Edward.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imetoa ufafanuzi kuhusu dawa za sh.bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa ya Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Muhimbili kama ilivyodaiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bungeni.

Bwanakunu alisema kuwa ripoti ya CAG ilionesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 na Bohari ya Dawa.

"Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.

Alisema kwamba baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na vifaa tiba vyote vilivyopokelewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo ambazo zilikwishapelekwa Muhimbili.

Aliongeza kuwa pamoja na juhudi za MSD imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na vifaa tiba vilivyopelekwa hospitalini hapo kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara ya kupeleka mali ambazo zote zipo MSD.

Akitolea ufafanuzi kuhusu picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za gari aina ya lori lenye herufi "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la MSD amesema nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.


Katika ripoti ya CAG ilionesha kwamba madawa na vifaa tiba ambavyo havikupokelewa kwa muda mrefu kutoka MSD vilikuwa vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 ambapo katika hali ya haikutajiwa kuchukua zaidi ya wiki moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi zao ziko Dar es Salaam.

Friday, April 29, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS VLADMIR PUTIN WA URUSI NA KUFUNGUA MKUTANO WA MAMBO YA FEDHA KWA WANAWAKE

SU4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
SU5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam  April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
SU6Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na Kimataifa Mhe. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam  April 28, 2016. Kwa ajili ya kuonana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi. Katikati Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
SU7Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu  mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa  April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR)
SU8Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu  mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR)
SU9

KAMPUNI YA SGA SECURITY YAGAWA VIFAA VYA USALAMA BARABARANI KWA WAENDESHA BODABODA MBEZI

SGS2SGS4Waendesha Bodaboda wakiwa wamejipanga mara baada ya kukabodhiwa msaada huo wa vifaa vya usalama barabarani.
SGS5Mkurugenzi wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA Security Bw. Eric Sambu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi  vikoti maalum vya usalama barabarani  kwa waendesha Bodaboda wa Mbezi Tangibovu jijini Dar es salaam wakati wakati kampuni hiyo ilipotoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni 4. Kulia ni Ofisa mwandamizi wa kampuni hiyo Bi. Sophia Kaihula.
……………………………………………………………………………………………………………KAMPUNI ya Ulinzi ya SGA imetoa msaada wa vifaa kusaidia waendesha bodaboda  Mtaa Mbezi A, katika kujiepusha na ajali katika siku  ya usalama  duniani.
Akizungumza wakati wa kakabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Erick Sambu amesema kuwa vifaa walivyopewa vitasaidia katika kujiepusha na ajali kutokana na dereva wa gari kuona kifaa hicho.
Amesema kuwa vifaa hivyo vina thamani ya sh.milioni Nne na kuahidi kuendelea kutoa msaada katika makundi mbalimbali kutokana na kazi yao ya kuangalia usalama.
Sambu amesema kuwa SGA  katika kuadhimisha siku ya usalama duniani na kuwataka wadau wengine kuunga mkono katika kuwangalia watu bodaboda.
Naye Mwakilishi wa Mwanyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbezi A, Carolyne Ngoda amesema kuwa SGA wameokoa maisha ya vijana wao wanaoshughuli na biashara ya kusafirisa watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Thursday, April 28, 2016

RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI MSAAFU AZINDUA RIPOTI YA MPANGO WA UHAMASISHAJI UWAZI KATIKA MAPATO YA MADINI, GESI ASILIA NA MAFUTA (TEITI)

Mwenyekiti wa mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI), Mark Bomani akimkaribisha Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh ili aweze kuzindua ripoti ya mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh akizungumza wakati wa uzinduzia  ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI)  jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) jijini Dar es Salaam leo akiwa na Mwenyekiti wa mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI), Mark Bomani na wengine ni wajumbe wa mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) wakiwa katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick akionyesha ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI)  jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua ripoti hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala wa Kampuni ya BDO Afrika Mashariki, Juvinal Betambila akifafanua jinsi ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) jijininDar es Salaam leo wakati wa kuzindua repoti hiyo.

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

bun1Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (kulia) wakati alipomuuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun3Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun4Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Kushoto ni Mbenge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
bun5Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kwahani na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi  (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge  mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Katikati ni Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun6Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Bariadi na Mwenyekiti wa Bunge Mtemi Andrew Chenge kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
bun7Mbunge wa Welezo, Saada  Salum Mkuya akichangia Bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

DOM1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
DOM2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
DOM3Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Dodoma kutokea mjini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

WAAJIRI WOTE WANAODAIWA MALIMBIKIZO YA MICHANGO YA NSSF WATAKIWA KULIPA MICHANGO KABLA YA JUNI 30

Bw. James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la  Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza na waandhishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo jengo la Benjamin Mkapa wakati akielezea kuhusu waajiri wanaodaiwa madeni sugu ya michango ya wafanyakazi wao na kutamka kwamba wasipolipa michango hiyo mpaka ifikapo Juni 30 mwaka huu shirika hilo linawapeleka mahakamani, kulia ni mmoja wa maofisa waandamizi wa shirika hilo Bw. Salim Khalifan pamoja na maofisa wengine wa shirika hilo waliohudhuria katika mkutano huo.
2Baadhi ya maofisa wa shirika hilo wakiwa katika mkutano huo.
_MG_5980Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa hiyo wakati Bw James Oigo Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Shirika la Taifa la  Hifadhi ya Jamii NSSF akizungumza nao katika mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………………………………
Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF) linapenda kutoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa malimbikizo ya michango ya wafanyakazi wao kulipa malimbikizo hayo kabla ya tarehe 30.06.2016.
Waajiri ni moja kati ya wadau  wakubwa wa shirika letu la NSSF kwa mujibu wa kifungu cha 11(6) na 12 (1) cha sheria ya NSSF, waajiriwa wana majukumu makubwa mawili.
  1. Kuhakikisha wafanyakazi wao wanaandikishwa katika shirika la taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mara tu wanapoajiriwa.
  1. Kuwakata michango yao asilimia 5% au 10% kutoka kwenye mshahara wa mwezi na kuwasilisha mchango huo ukiwa ni asilimia 20% ya mshahara wa mwezi, maana yake ni kwamba mwajiri baada ya kufanya makato kutoka katika mshahara wa mfanyakazi wake, anatakiwa kuongeza asilimia 10% au 15% ili ifikie asilimia 20% na kuwasilisha kwenye shirika.
Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya NSSF no 28 ya mwaka 1997, waajiri wote wanatakiwa wawasilishe michango ya wafanyakazi wao ndani ya siku 30 toka tarehe ya mwisho wa mwezi husika, kwa mfano mchango wa mwezi machi,2016 , unatakiwa uwe umewasilishwa kwenye shirika kabla ya tarehe 30/4/2016 kinyume na hapo ni ukiukwaji wa sheria na ni kosa la jinai.
Lakini kuna baadhi ya waajiri kwa sababu wanazozijua wenyewe, wanashindwa kutekeleza hitaji hili la kisheria kikamilifu kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Kitendo cha kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao  kwa wakati si tu kwamba ni kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 72 (d) cha sheria ya NSSF na ambayo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha miaka 2 jela, lakini pia ucheleweshaji huu unasababisha madhara makubwa kwa wanachama na shirika kwa ujumla.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...