Monday, June 09, 2014

PICHA MBALIMBALI ZA HARUSI YA MBUNGE WA ARUMERU-MASHARIKI- CHADEMA JOSHUA NASSARI NA ANANDE NNKO ILIVYOFANYA,MSAFARA WAPITA BARABARA KUU MAMIA WAJITOKEZA KUMPONGEZA

 Msafara ukaanza safari ya kuelekea barabara kuu ya Moshi/Arusha ukitokea kanisani Kilinga.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki-Chadema , Joshua Nassari na ,Anande Nnko
wakiwa ndani ya gari muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la Kilinga wilayani Arumeru tayari kwa kuelekea viwanja vya  Usa-River Academy.
Bi Harusi Anande Nnko akiwa katika gari tayari kuelekea katika viwanja vya Usa-River Academy.

 Baadae maharusi wakabadili gari ili waweze kuonekana vyema na wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki.
Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani
 Mharusi waki "Show Love"
Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani.
 Mamsapu akianza majukumu ya kuhakikisha Mzee anakuwa nadhifu kila wakati.

Wednesday, June 04, 2014

Picha Mbalimbali Za Mazishi ya Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini -Chadema Zitto Kabwe Mjini Kigoma


  Mbunge wa Kigoma Kaskazini  Zitto Kabwe akiwa Mbele ya Kaburi la Mama yake mzazi Bi 
Shida Salum muda mfupi baada ya kuzikwa jana kwenye makaburi ya Rubengela mjini Kigoma 
  Umati wa wananchi wa mkoa kigoma na viongozi kutoka mikoa mbalimbali wakielekea makaburini tayari kwa mazishi ya Shida Salum Mama mzazi wa mbunge wa Kigoma Kaskazini  Zitto Kabwe.
  Wananchi waliohudhuria mazishi ya shida Salum Mama yake Mzazi Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu huyo wakielekea makaburi ya Rubengela mjini Kigoma kwa mazishi.


 Mbunge wa Rombo(CHADEMA), Mhe. Joseph Selasini(Kulia)Mbunge wa Kigoma Mjini-CCM Peter Serukamba(wa pili Kushoto)wakiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe (katikati)wakielekea kwenye mazishi ya mama Mzazi wa Mheshimiwa Zitto kabwe bi Shida Salum mjini Kigoma 

 Mbunge wa Kuteuliwa na Rais James Mbatia(wa tatu kushoto)akijadilia jambo na mwenyekiti wa Chama cha wananchi(CUF)Profesa ibrahim Lipumba wa tatu kushotokwenye mazishi ya mama Mzazi wa Mheshimiwa Zitto kabwe bi Shida Salum mjini Kigoma Jana
Baadhi ya Wabunge wakiwa katika msiba wa mama mzazi wa Mbunge mwenzao Zizzto Kabwe (wapili kushoto aliyefuatana na baba yake Zuberi Kabwe) mjini Kigoma na Juu ni Kaburi alipo zikwa mama mzazi wa Zitto Kabwe.

Monday, June 02, 2014

Wafanyakazi wa Airtel watoa msaada hospitali ya Ocean Road



Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba (kulia), akikabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’ mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.

Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba (kulia), akikabidhi msaada wa moja kati ya ‘wheel chair’ mbili, machela za kisasa mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.
Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule (kulia) akiwaongoza wanachama wa kikundi cha wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakati walipotembelea wagonjwa wa taasisi hiyo, baada ya kukabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’ mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanachama wa kikundi cha wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakiwa wamebeba bidhaa mbalimbali, walipotembelea wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na kukabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, wheel chair mbili vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwaajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakibadilishana mawazo na Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule.
Picha ya pamoja baada ya kukabidhi vifaa hivyo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia umoja wa wanawake ujulikanao kama Airtel Divas umetoa msaada wa vifaa vya hospitali kwaajili ya wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya saratani katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es salaam

Msaada huu unafatia harambee kwa ajili ya kuchangisha pesa iliyofanywa na Airtel Diva mwezi uliopita kwaajili ya kupata fedha za kuwasaidia wagojwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya kansa katika hospitali ya Ocean Road.

Akiongea wakati wa kutoa msaada huo mwenyekiti wa Airtel Divas Amitin Mbamba alisema” Tunatambua na tunapokea kwa machungu matatizo yanatowapata wanawake na watoto wanaougua saratani na katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2014 tuliamua kuchangisha pesa kwaajili yakutuwezesha kununua vifaa vya hospitali na kuwasaidia wanawake na watoto  pamoja na wagonjwa wengine hospitalini hapa. Na leo tunayofuraha kutoa stretcher 2 pamoja na wheelchair 2 zenye thamani ya shilingi million 5 hospitalini hapa.”

Tunaamini msaada huu utawawezesha wahudumu kupata nyenzo muhimu na kuweza kufanya kazi yao ya kutoa huduma kwa wagojwa kwa ufanisi zaidi.

“Nia yetu ni kuhakikisha tunaendelea kutoa muda wetu na rasilimali katika kushikiri na kuchangia shughuli za huduma kwa jaimii ili kukubailiana na matatizo yanayoikumba jamii inayotuzunguka hususani wanawake wenzetu” aliongeza Mbamba

Mmoja ya wajumbe wa Airtel Divas Bi Deliphina Martin Msuya alisema” tunayofuraha kuwa sehemu ya kutoa msaada kwani tunatambua umuhimu wa wanawake katika kusimamia familia,  inagusa sana kuona jinsi gani wanawake wenzetu wanavyougua au kuuguza watoto wao hospitalini hapa hivyo tunatoa wito kwa wanawake wengine huku nje mmoja mmoja au kwa makundi kuwasaidia wanawake wenzetu walio katika changamoto hizi kwani ni jukumu letu kusaidia wahitaji.

Akiongea mara ya kupokea msaada huo Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule alisema” Hospitali yetu inaupungufu wa vifaa mbalimbali zinavyotuwezesha kuhudumia wagonjwa tunashukuru sana Airtel kwa msaada wao na kwa kuwezesha kupata hivi vifaa kwani vitatusaidia katika kutoa huduma na kuongeza ufanisi wa kazi zetu za kusaidia wagonjwa hapa hospitalini. Nachukua nafasi hii kuwaomba makampuni mengine na vikundi mbalimbali kusaidia changamoto zingine zilizopo hospitalini hapa.

Airtel Divas ni mpango ulioanzishwa Airtel Afrika nzima wenye lengo la kuwahamashisha na kuwawezesha wanawake wanaotoka katika makuzi , mila na tamaduni mbalimbali kujiamini na kufanikiwa katika maisha , mpango huu ulizindulia Airtel Tanzania March 2012.

MWIGULU NCHEMBA AMPANIA MBUNGE MSIGWA JIMBONI ASEMA ATAONGOZA MAPAMBANO YA KUMNG'OA


Naibu katibu mkuu wa CCM bara Mwigulu Nchemba akiwahutubia  wananchi wa  jimbo la Iringa mjini.
Vijana wa CCM wakifurahia  hutuba ya Nchemba
Wananchi  wa  jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza Nchemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa

Viongozi  mbali mbali wa CCM mkoa  wa Iringa

Nchemba akipongezwa na kada wa CCM kutoka chuo cha Mkwawa
Kamanda  wa UVCCM mkoa  wa Iringa Salim Asas wa pili kulia akiwa na viongozi mbali mbali
Nchemba  akiwaaga  wana Iringa
Na Francis Godwin Blog
NAIBU katibu mkuu wa  chama cha mapinduzi (CCM) Bara Mwigulu Nchemba awahakikishia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini kuwa  muda wa mbunge wa  jimbo hilo kuongoza umefika kikomo na kuwa ataongoza mapambano ya kumng’oa mwakani katika uchaguzi mkuu.

Akiwahutubia  wananchi  wa jimbo la Iringa mjini leo katika uwanja wa Mwembetogwa Nchemba ambae ni naibu  waziri wa fedha  alisema  kuwa mbali ya mbunge  huyo kupewa nafasi hiyo ya bure mwaka 2010 ila bado ameshindwa kuwa na huruma na wananchi wa  jimbo hilo na kuendelea kujinufaisha yeye badala ya kuwekeza kwa  wananchi hasa  vijana na ndio  sababu ya kushindwa kufanya vikao na wanachama wake na kuendelea kuitisha maandamano badala ya kufanya kazi.

“Tutajipanga  vema kila kona ya jimbo la Iringa mjini ili kulirudisha jimbo mikononi mwa CCM kwa  kumpata mbunge ambae  atawatumikia  wananchi na sio wa kujitumikia yeye na kuwa mbunge wa maandamano kwa kipindi chake  chote”

Nchemba  alisema  kuwa kutokana na kazi  kubwa iliyopfanywa na vijana wa jimbo la Iringa kwa kumpigania mbunge Msigwa alipaswa  kuwa na roho ya huruma kwa vijana hao ikiwa ni pamoja na kuwageuza daraja na kuwafanyisha maandamano yasiyo kwisha badala ya kuwaanzishia miradi ya kiuchumi.

“Hivi tazameni leo maeneo  yote ya makanda wa Chadema majimboni mwao ni maandamano kila siku kila wakati utasikia hakuna kulala makamanda huku mbunge anashindwa kuwasaidia …..na siku hizi wanakuja na hoja  ya makamanda pambaneni tutachukua nchi huku hata kata kwao ni ndoto  sasa niwaambie  leo hata nusu ya nchi hii kamwe  hawatapata”

Asema  mmoja kati ya mke wa  kiongozi mojawapo wa Chadema alimuuliza hivi kwa nini mume wake anapenda  sana maandamano alimjibu  kuwa mume  wake huyo akichukia huwa anafanya maandamano ndani ya chumba cha  kulala.
Nchemba  pia ameponmgeza  utendaji kazi wa mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na kuwa  siku  zote  amekuwa akiwapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini bungeni tofauti na mbunge wa jimbo mchungaji Msigwa ambae amekuwa akiongoza kwa kufanya maandamano.

Katika hatua  nyingine Nchemba  alisema amesema kuwa muda wa matajiri kuendelea  kujinufaisha na misamaha ya kodi  umekwisha na  kuwa anajipanga kupeleka sheria bungeni itakayowabana wafanyabiashara wakubwa kulipa kodi kama  wanavyolipa wafanyabiashara  wadogo.

Alisema kuwa  watu  wanapata misamaha  hadi inakatisha tamaa kwani ni pesa nyingi za kimaendeleo zinapotea  kutokana na utitiri wa misamaha inayoendelea kutolewa .

“Napeleka sheria katika bunge  hili la bajeti itakayofuta misamaha ya kodi kwa viwanda na wafanyabiashara  wakubwa…inakuweje  wananchi masikiti hata wanapotaka kuanzisha  saluni wanalipizwa kodi ila wafanyabiashara  wakubwa na baadhi ya  watu pia nitapeleka sheria ya kubana matumizi ya  fedha za umma”

Alisema kuwa inashangaza  kuona mashirika ya umma yanavuna na kutumia huku wanyonge wakiendelea  kuteseka na walimu na askari  wakiendelea kukosa kulipwa madai yao.

“hatuwezi  kusema  leo  walimu ama  askari ni wengi  wakati watu  wanakwepa kulipa kodi huku  wanafunzi  wakikosa mikopo ya elimu ya juu eti kutokana na kukosa fedha  wakati watu  wengine  wanakwepa kodi….hili ni jambo la aibu sana najua  wapo wabunge  watakaopinga ila  wananchi mtaona ni nani ni mbunge wa wananchi …kwani najua wapo  wabunge ambao hawalipendi hili watapinga ila lazima nilifikishe hata kama chungu ila lazima suala hili likomeshwe”

MTUHUMIWA WA “KUFUTA MADENI” YA MIKOPO AKIRI KOSA, AHUKUMIWA KIGOMA

KIGOMA, Septemba 4, 2026 — Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma imemhukumu Nicholaus Komba Mahitana maarufu kama Abdallah Mahimbo baad...