●Wadau wa chumvi kuanza kuuza chumvi iliyochakatwa
●Zaidi ya tani 60 hadi 100 kuchakatwa kwa mwezi
●Wazalishaji wa chumvi waipongeza serikali kwa utatuzi wa changamoto
Dodoma
Katika juhudi za kuendeleza na kuboresha uzalishaji wa madini chumvi nchini Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ipo mbioni kukamilisha kiwanda cha kuchakata madini chumvi kilwa mkoani Lindi pamoja kusaidia ujenzi wa viwanda mkoani Tanga na Mtwara.
Hayo yameelezwa leo Aprili 23, 2026 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde wakati wa kikao baina ya Chama cha Wazalishaji Chumvi Tanzania (TASPA) na Wizara ya Madini na taasisi zake kilichofanyika jijini Dodoma.
Waziri Mavunde , amesema kuwa, Serikali ilipokea maombi ya TASPA na kufanikiwa kushusha mrabaha katika madini chumvi kutoka asilimia 4 mpaka asilimia 1 ya bei elekezi.
Waziri Mavunde ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kushughulikia uanzishwaji wa leseni moja katika shamba moja lengo ni kutofautisha na madini mengine ikiwa pamoja kuongeza uzalishaji wa chumvi bora nchini.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika ya Madini la Taifa (STAMICO) Dkt.Venance Mwase amesema kuwa miundombinu ndani ya kiwanda yamekamilika kwa asilimia kubwa.
Dkt. Mwase ameongeza kuwa , kiwanda kitakuwa na uwezo wa kupokea chumvi ghafi kutoka kwa wazalisha kuanzia 50 hadi 60 kwa siku.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TASPA Bi. Hawa Ghasia ameishukuru Serikali kwa kuwezesha mazingira bora ya uvunaji wa chumvi ikiwa pamoja na kupanda kwa bei ya chumvi baada ya kuwepo kwa zuio la uingizwaji wa chumvi ghafi kiholela kutoka nje ya nchi.
Kiwanda cha kuchakata chumvi mkoani Lindi pindi kitakapoanza kazi kinatarajia kuchakataji tani 60 hadi 100 kwa siku.





No comments:
Post a Comment