Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria kwa njia ya mtandao, tarehe 11 Aprili, 2026 Ikulu, Dodoma.
Mhe. Rais ametunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu ya Heshima kwa kutambua mchango wake kama Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afya ya Mama na Mtoto, Taswira nzuri katika masuala ya Uongozi kwa Wanawake Afrika na Kusimamia Masuala ya Biashara hususani kwa Vijana Afrika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya mtandao na Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria ambacho kimemtunuku Shahada ya Uzamivu ya Heshima , tarehe 11 Aprili, 2026 Ikulu, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima na Nasarawa State University kwa njia ya mtandao, katika hafla iliyofanyika tarehe 11 Aprili 2026, Ikulu jijini Dodoma.
Tuzo hiyo imetolewa kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza ajenda za kijamii na kiuchumi barani Afrika, hususan katika maeneo ya nishati safi ya kupikia, afya ya mama na mtoto, pamoja na kukuza taswira chanya ya uongozi wa wanawake.
Aidha, Mhe. Rais ametambuliwa kwa juhudi zake za kusimamia na kuhamasisha maendeleo ya biashara, hasa kwa vijana, ambapo amekuwa kinara wa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji na ujasiriamali.
Kutunukiwa kwa heshima hiyo kunadhihirisha nafasi ya Tanzania katika ramani ya uongozi bora barani Afrika, pamoja na mchango wa Mhe. Rais katika kuleta mageuzi yenye tija kwa jamii na vizazi vijavyo.





No comments:
Post a Comment