Wednesday, April 22, 2026

NHC NA SCOUT TANZANIA WAIMARISHA USHIRIKIANO KUPITIA UBIA







Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kupanua wigo wa ushirikiano wake kwa taasisi mbalimbali baada ya kufanya kikao maalum na viongozi wa Scout Tanzania, kikilenga kujadili fursa za ubia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kikao hicho kiliwakutanisha viongozi wa ngazi ya juu kutoka Scout Tanzania akiwemo Mwenyekiti wa Bodi, Bethi Mkwasa, pamoja na wajumbe wa bodi Juma Dossa na Marry. 

Wengine waliohudhuria ni Kamishna wa Scout Tanzania, Hellen Mkami, pamoja na wajumbe wa kamati ya ubia, akiwemo Nassoro Abubakari.

Katika kikao hicho, viongozi hao walipata ufafanuzi wa kina kuhusu namna ambavyo NHC inatekeleza miradi kupitia mfumo wa ubia (PPP), ikiwemo aina mbalimbali za ubia zinazotekelezwa, taratibu za kuingia ubia, pamoja na vigezo vinavyotumika kuchagua washirika.

Aidha, faida za kuingia ubia na NHC zilielezwa kwa kina, zikiwemo uendelezaji wa ardhi kwa tija, uhakika wa uwekezaji wenye tija, pamoja na mchango wake katika kukuza uchumi na huduma za kijamii.

Kikao hicho kimeelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kujenga msingi wa ushirikiano madhubuti kati ya NHC na Scout Tanzania, unaotarajiwa kufungua fursa mpya za uwekezaji na maendeleo yenye manufaa kwa pande zote pamoja na jamii kwa ujumla.

No comments:

NHC NA SCOUT TANZANIA WAIMARISHA USHIRIKIANO KUPITIA UBIA

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kupanua wigo wa ushirikiano wake kwa taasisi mbalimbali baada ya kufanya kikao maalum na viongo...