Saturday, January 26, 2019

MATEMBEZI YA KUIMARISHA AFYA YA NHC YAFANA, MKURUGENZI MKUU ATOA MAAGIZO MAZITO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Abdallah Banyani akizungumza na wafanyakazi wa NHC (hawapo pichani) muda mfupi mara baada ya kumaliza matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yaliyoanzia jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House kuelekea Barabara ya Barack Obama hadi Palm Beach na kuingia Barabara za Ali Hassan Mwinyi, Ohio, Kivukoni Front, Luthuli na baadaye kuelekea kwenye eneo kutakakokuwa na mazoezi ya viungo katika eneo la Sea View Beach (Dengu Beach). Dk Banyani amehimiza matembezi hayo kufanyika kila mwisho wa mwezi na kwa mikoa yote ya NHC ili kuimarisha afya za wafanyakazi na kujenga mshikamano.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Abdallah Banyani akiongoza matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yaliyoanzia jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Abdallah Banyani akiongoza matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yaliyoanzia jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Abdallah Banyani leo ameongoza matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yakianzia leo na kuendelea.

Akizungumza muda mfupi mara baada ya kuhitimisha matembezi hayo ya umbali wa kilomita 4.5  yaliyoanzia jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House kuelekea Barabara ya Barack Obama hadi Palm Beach na kuingia Barabara za Ali Hassan Mwinyi, Ohio, Kivukoni Front, Luthuli na baadaye kuelekea kwenye eneo kutakakokuwa na mazoezi ya viungo katika eneo la Sea View Beach (Dengu Beach) alisema matembezi hayo yatakuwa ya kila mwezi.

"Kwanza ninawahukuru kwa kufika hapa leo hii lakini niseme leo hapa kwamba hii ndo itakuwa kawaida yetu, yatakuwa maisha yetu na ni lazima kwaajili ya kutunza afya zetu, tunataka kuwa na wafanyakazi wenye afya njema, hivyo wale wa kule Mwanza, Arusha na kwingineko tunavyotembea sisi na wao watembee ni wajibu wetu,"alisema Dk Banyani.

Alisema kuwa matembezi hayo yana malengo matatu, kwanza ni kutekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, pili kuimarisha afya na utimamu wa mwili na  tatu ni kujenga ushirikiano wa kikazi na hivyo kuongeza ufanisi ndani ya Shirika.

Matembezi ya Mwezi huu yamefanyika leo Jumamosi ya tarehe 26/01/2019 kuanzia saa moja asubuhi na kujumuisha wafanyakazi wa Shirika tu na kuwashirikisha pia Upanga, Ilala, Kinondoni na Temeke.

Mkurugenzi Mkuu alisema matembezi hayo yatafanyika Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi popote pale watumishi wa NHC walipo na kwamba huu ni mwanzo na huko siku za mbele kutakuwa na michezo mingi zaidi.


Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi yaliyoanzia jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House.
 Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakiwa katika barabara ya OHIO.
  Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakiwa katika barabara ya LUTHULI.
  Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakiwa katika barabara ya BARACK OBAMA .
   Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakiwa katika barabara ya BARACK OBAMA .
   Wafanyakazi wakiwa wakiwa katika mazoezi ya kukamilisha matembezi hayo.
 Wafanyakazi wakiwa wakiwa katika mazoezi ya kukamilisha matembezi hayo.


 Kabla ya kuondoka kuanza matembezi.

Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakianzia matembezi hayo katika barabara ya BARACK OBAMA kuelekea barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

 Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakiwa katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
  Wafanyakazi wakiwa katika ari wakifanya matembezi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakiwa katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk. Maulidi Abdallah Banyani akiongoza matembezi katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

 Matembezi yakiwa yanapita katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi mbele ya jengo la makao makuu ya NHC Kambarage House.




 Wafanyakazi wakiwa wakiwa katika mazoezi ya kukamilisha matembezi hayo chini ya Mwalimu wa mazoezi wa Shirika JOE.
Wafanyakazi wakiwa wakiwa katika mazoezi ya kukamilisha matembezi hayo chini ya Mwalimu wa mazoezi wa Shirika JOE.
   Wafanyakazi wakiwa wakiwa katika mazoezi ya kukamilisha matembezi hayo chini ya kocha JOE.



No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...