Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani leo amekutana na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai na kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo. Spika Ndugai ameeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji miradi inayofanywa na Shirika na akahimiza kasi hiyo iongezwe ili kuwapatia Watanzania wengi zaidi huduma ya nyumba hususani wale wa Dodoma yalipo makao makuu ya nchi.
Spika akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu, Dk Banyani.
Dk. Banyani akitoka nje ya jengo la bunge baada ya kukutana na Spika Ndugai.Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu Dk Banyani (wa pili kulia) baada ya mkutano huo.
Spika Ndugai akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.
Mjadala ukiendelea baina ya pande mbili hizo.
Wakifurahia jambo baada ya majadiliano ya hoja kadhaa za maendeleo ya sekta ya ujenzi na Shirika kwa ujumla.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Yahya Charahani akizungumza jambo mbele ya Spika Ndugai.
Mjadala ukiendelea na Spika Mheshimiwa Job Ndugai wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Banyani (wa Kwanza Kulia) akitoka nje ya jengo la bunge baada ya kukutana na Spika Ndugai. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo na Masoko, Itandula Gambalagi (wa kwanza kushoto) na katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.
No comments:
Post a Comment