Thursday, January 31, 2019

MKURUGENZI MKUU ATEMBELEA ENEO JIPYA KUNAKOKUSUDIWA KUJENGWA MAKAZI YA WATUMISHI WAANDAMIZI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani jana alitembelea eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu.  Eneo lipo karibu kabisa na ulipo mji wa Serikali kulikojengwa wizara mbalimbali za Serikali. Pichani Afisa Miliki wa NHC Dodoma Jaffari Chege akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu mfano wa michoro ya eneo hilo. 
 Ukamilishaji wa ujenzi wa mji wa kiserikali ukiendelea ndani ya jengo la Wizara ya Fedha wakiwa wanafanya skimming.
 Jengo la Wizara ya Fedha lilivyo sasa.

Eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu.
 Kaimu Mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa Abdallah Migilla akiteta jambo na Injinia Hassan Mohammed wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye eneo kunakojendwa wizara ya Viwanda na Uwekezaji.
 Mkurugenzi Mkuu akitembelea eneo la wizara hizo

 Mkurugenzi Mkuu akielekeza jambo.

 Eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu.

Umaliziaji ukiendelea katika wizara ya Viwanda na Uwekezaji 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...