Monday, January 01, 2018

JK AUKARIBISHA MWAKA MPYA 2018 NA WANANCHI WA MSOGA, MKOANI PWANI USIKU WA JANA

 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgallu, sambamba na wananchi wa mji wa Msoga Mkoani Pwani kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya wa 2018 katika hafla iliyoandaliwa na Dkt. Kikwete kijijini kwake Msoga.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia fataki angani wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, iliyofanyika usiku huu kijijini kwake Msoga, Mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (aliyemshika mtoto) alikuwa ni mmoja wa wakazi wa mji wa Msoga waliojumuika nyumbani kwa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kulikofanyika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2018.
 Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa heri ya mwaka mpya na baadhi ya wageni waliofika kijijini kwake hapo.
 Msanii wa Muziki wa Singeli, Msaga Sumu akitumbuiza mbela ya maelfu ya wananchi wa Msoga katika sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2018, iliyofanyika Nyumbani wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, Msoga Mkoani pwani.
 Burudani ya Ngoma ya Asili.
 Burudani ya Utamaduni wa Kimaasai.

















No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...