Wednesday, June 21, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU MLANDIZI MKOANI PWANI PIA AZINDUA VIWANDA VINGINE MKOANI HUMO


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kuzindua rasmi Mradi wa huo wa Upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Ruvu juu Mlandizi Mkaoni Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Archard Mutalemwa  mara baada ya kuzindua mradi huo Mkubwa wa maji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji ya Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Eng. Cyprian Luhemeja akitoa maelezo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya Pwani na Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ujumbe aliotumiwa na Waziri mkuu wa India Narendra Modi kupitia Luninga kabla ya kudua Mradi huo wa maji.
 Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kabla ya kufungua kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akipeperusha bendera kuashiria kuiruhusu treni ya TRL kusafirisha nondo kutoka kwenye kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli   pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda hicho cha nondo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi kwenye sehemu ya kiwanda cha kutengeneza  matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua Mradi wa maji wa Ruvu juu Mlandizi mkoani Pwani.
PICHA NA IKULU

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...