Thursday, June 08, 2017

BULEMBO AFUNGA KAZI WILAYA YA MISENYI NA BUKOBA MJINI MKOANI KAGERA

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Misenyi, Mabalozi, viongozi wa Jumuia za CCM na watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo mkoani Kagera.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwaili ukumbini
 Wajumbe wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza Alhaj Bulembo
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzana, Wilaya ya Misenyi Rehema Mtawala akimkabidhi zawadi maalum Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo kabla ya kikao kuanza
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akionyesha zawadi hiyo maalum baada ya kukabidhiwa. Zawadi hiyo ina maneno ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mbunge. 
 Mwenyekiti wa CCM wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Haji Seruhu akifungua kikao hicho
 Katibu wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Mwajuma Mboha, akieleza maneno ya utangulizi katika kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misenyi Haji Seruhu, wakati wanapita taarifa iliyosomwa na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo
 Wajumbe wakihamasika kwenye kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akitulia kumsikiliza kwa makini mshairi Mansur Athan wakati akighani shairi mwishoni mwa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea zawadi ya Mbuzi aliyopewa na Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Misenyi wakati wa kikao hicho leo.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera  Yahya Kateme (kushoto) akibadilishana mawazo na Vijana wa wa CCM nje ya ukumbi baada ya kikao
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ajhaj Abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza nje ya ukumbi badhi ya wadau waliotaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo baada ya kikao hicho 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwafafanulia jambo nje ya ukumbi baadhi ya wadau  
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza wadau hata baada ya kupanda gari lake tayari kwa kuondoka
Baada ya wadau kuridhika wakamuaga kwa furaha na kumtakia safari njema kwenda Wilaya ya Bukoba mjini
 Safari ya Alhaj Bulembo kutoka Misenyi kwenda Wilaya ya Bukoba mjini ilipitia kwenye daraja hili la Mto Kagera, eneo la Kyaka.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera  Yahya Kateme akizungumza na vijana waendesha bodaboda aliowakuta Bukoba Mjini, baada ya msafara wa Alhaj Abdallah Bulembo kuwasili
 Mwenyekiti huyo wa UVCCM akapiga picha ya pamoja na vijana wa green Guard wa Bukoba mjini
 Baada ya kuwasili tu Bukoba Mjini, Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo alieanda ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu na kuwa na mazungumzo naye kwa muda. Pichani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo hayo. Wengine kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Lahel Ndegeleki na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Costansia Buhiye
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimweleza jambo Mkuu huyo wa mkoa kabla ya kuondoka 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia vijana wa green Guard nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa.
KIKAO BUKOBA MJINI🔽
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimwelekeza jambo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini Yusuf Ngaiza wakati wa kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya hiyo, Mabalozi, viongozi wa Jumuia na Watendaji wa serikali.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera Yusuf Ngaiza akifungua kikao hicho
 Wajumbe wakiwa ukumbini katika kikao hicho
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho Bukoba mjini mkoani Kagera. PICHA; BASHIR NKOROMO

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...