Saturday, January 14, 2017

PICHA MBALI MBALI ZARAIS MAGUFULI ALIVYOFUNGUA VIWANDA VIWILI MKOANI SHINYANGA

Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ijumaa Januari 13,2017 amefungua rasmi viwanda viwili mkoani Shinyanga. 

Rais Magufuli amefungua Kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited na kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda,juisi na maji. 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Katikati ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company limited kilichopo katika manispaa ya Shinyanga,kulia ni mkurugenziwa kiwanda hicho Freddy Shoo.
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited kilichopo katika manispaa ya Shinyanga
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia kwa kuwapungia mkono wananchi wa mkoa wa Shinyanga waliofika katika kiwanda Fresho Investment Company Limited kushuhudia uzinduzi rasmi wa kiwanda hicho 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kiwanda hicho.Kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kushikana mkono na mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company limited Freddy Shoo baada ya kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa kiwanda hicho
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kukata utepe kuashiria kufungua rasmi kiwanda cha kutengeneza mifuko ya sandarusi cha Fresho Investment Company Limited.
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited cha Mkoani Shinyanga.Kushoto wa kwanza kushoto ni mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele,wa tatu ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Wa kwanza kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akifuatiwa na mbunge wa jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi,mkurugenzi wa kiwanda hicho Freddy Shoo
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kiwanda cha Fresho Investment Company Limited akiongozwa na mkurugenzi wa kiwanda hicho Freddy Shoo
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company Limited Freddy Shoo (kushoto) akimwonesha rais Magufuli jinsi uzalishaji wa vifungashio/mifuko ya sandarusi unavyofanyika katika kiwanda hicho
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli akiangalia mifuko ya sandarusi katika kiwanda hicho
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli akiangalia mifuko/vifungashio vya bidhaa mbalimbali vilivyotengenezwa katika kiwanda hicho
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company Limited Freddy Shoo akimwelezea rais Magufuli namna mitambo ya kisasa iliyopo katika kiwanda hicho inavyofanya kazi katika kiwanda hicho
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company Limited Freddy Shoo akiteta jambo na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha Kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited ambapo alisema kiwanda hicho ni kizuri na cha kisasa huku akimpongeza mmiliki wa kiwanda hicho Freddy Shoo ambaye ni Mtanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Viongozi mbalimbali wakimsikiliza rais Magufuli ambaye alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania wengine wenye pesa kujitokeza kuwekeza katika viwanda ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakua na wananchi wanapata ajira
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Tunamsikiliza rais Magufuli
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Viongozi mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (mwenye ushungi mweupe katikati) wakimsikiliza rais Magufuli
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blogHapa ni ndani ya kiwanda cha kutengeneza vinywaji baridi ikiwemo soda,maji na juisi cha Jambo Food Products Company Limited.Katikati ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mitambo ya kisasa iliyopo katika kiwanda hicho ambacho awamu ya kwanza ya ujenzi wake ulianza mwaka 2015 na kukamilika Juni 2016 kwa kuanza na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda,Malta,Fresh Juice,Energy drinks na maji kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 200 kwa siku 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Kushoto ni mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akimweleza rais Magufuli namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi.Pamoja na mambo mengine alisema awamu ya pili ya ujenzi itakamilika Oktoba 2017 ambapo kiwanda hicho kitaweza kusindika na kufungasha matunda yote yaliyopo kanda ya ziwa Victoria
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi ambaye ni mbunge wa Meatu mkoani Simiyu akimwelezea rais Magufuli jinsi mfumo wa komputa unavyofanya kazi katika shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho cha vinywaji baridi 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli akiwa katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited cha mkoani Shinyanga ambacho asilimia 100 ya umiliki wake ni watanzania wazawa
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blogRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia soda zilizozalishwa katika kiwanda hicho zikiwa tayari kwa ajili ya matumizi
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akitoa hotuba fupi kuhusu kiwanda hicho.Alisema uwekezaji utakapokamilika mwezi Oktoba mwaka huu,utakuwa na thamani ya dola 125,000,000.Mbuzi aliwataja waliofanikisha katika ujenzi wa kiwanda hicho kuwa ni Benki ya CRDB (Tanzania),COMMERZ Bank (Germany),Krones (Germany),Volvo(Tanzania) na EKN Bank ( Sweden) 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Mbuzi alimshukuru rais Magufuli kufungua kiwanda hicho na kuahidi kuendelea kuunga mkono kwa vitendo jitihada za serikali ya awamu ya tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Wananchi wakimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Mbuzi ambapo alisema tayari kiwanda hicho kimetoa ajira rasmi 365 na zisizo rasmi 500 na matarajio ni kufikia ajira 2500 pindi uwekezaji utakapokamilika na kwamba hivi sasa bidhaa zao wanauza ndani ya nchi na wanatarajia kupanua masoko ya nje ya nchi kwa nchi za Burundi,Rwanda na Kongo
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited ambapo aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kumuunga mkono kwa vitendo kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya viwanda badala ya kuendelea kutegemea viwanda vya nje ya nchi. 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alieleza furaha yake kuona mkoa wa Shinyanga ukiwa kituo cha uzalishaji wa vinywaji huku akiwapongeza viongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuunga mkono kwa vitendo na kuahidi kuwasaidia wawekezaji wazawa kupata mikopo katika benki mbambali ili wawekeze zaidi wananchi wapate ajira
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli alisema wawekezaji wazawa katika viwanda viwili alivyovifungua mkoani Shinyanga wameonesha uzalendo wa kweli kwa nchi yao na kuwataka watanzania kutoogopa kuanzisha viwanda hata kama vingekuwa vidogo namna gani
Wananchi wakimsikiliza rais Magufuli
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam ambaye pia ni mwenyekiti wa ALAT taifa wakimsikiliza rais Magufuli 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Wa kwanza kulia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa na mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Mbuzi wakifuatilia hotuba ya rais Magufuli
Wananchi wakimsikiliza rais Magufuli
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Katikati ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa na askari polisi wakati rais Magufuli akizungumza katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigawa soda kwa wananchi zilizozalishwa katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kilichopo katika manispaa ya Shinyanga 
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wakati akigawa soda kwa wananchi zilizozalishwa katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli akiendelea kugawa soda kwa wananchi
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigawa soda kwa viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kugawa soda
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli akiendelea kugawa soda
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais Magufuli akigawa soda kwa kikundi cha wacheza ngoma
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinywa soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited cha mkoani Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia utamu wa soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
Wananchi wakiwa wamesimama baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuondoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited baada ya kufungua kiwanda hicho
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...