JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
MAOMBI YA NAFASI 1000 ZA MAFUNZO YA STADI ZA KUTENGENEZA VIATU
1. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza Programu ya Kukuza Stadi za Kazi Nchini ya miaka mitano (2016 -2021) ambayo imelenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Hivyo, OWM-KVAU imeingia makubaliano na
Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam Kampasi ya Mwanza iliyo eneo la Ilemela Mwanza, kutoa mafunzo ya stadi za kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi. Lengo ni kuhakikisha nchi inakua na nguvu kazi ya kutosha yenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira katika kutengeneza bidhaa za ngozi nchini.
2. Ofisi inapenda kutangaza nafasi 1,000 za mafunzo yatakayoanza ifikapo tarehe 20 Februari, 2017 katika Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam Kampasi ya Mwanza. Vijana wa Kitanzania, wenye elimu ya msingi na kuendelea na umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo wawasilishe maombi yao kuanzia tarehe 22/ 01/2017 hadi 04/02/2017 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:
(i) Barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe;
(ii) Nakala ya Cheti cha Elimu uliyohitimu
(iii) Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura;
(iv) Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa anaoishi mwombaji; na
(v) Picha nne za paspoti.
3. Maombi yawasilishwe kwa Mkuu wa Kampasi, TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM – KAMPASI YA MWANZA, S.L.P. 2525, Mwanza au kwa barua pepe: info@mwanzacampus.dit.ac.tz
4. Watakao kuwa na sifa na vigezo wataitwa kwenye usaili kuanzia tarehe 8 hadi 11 Februari, 2017.
IMETOLEWA NA:
KATIBU MKUU
18 Januari, 2017
No comments:
Post a Comment