Sunday, January 29, 2017

MABEHEWA ZAIDI YA MATANO YA TRENI YA MWENDO WA HARAKA (DERUXE) YAANGUKA PWANI IKITOKEA KIGOMA KUJA DARÅ™


Baadhi ya Mabehewa ya  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.
 Baadhi ya Mabewa mengine yakionekana kuacha njia

Baadhi ya Abiria waliokuwa wamependa  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam,wakitoka kwenye mabehewa hayo mara baada ya kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinaeleza kuwa takriban mabehewa 10 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea,aidha imeelezwa kuwa watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa. 

Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio. 

“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez. 

Taarifa zaidi zitawajia kadri zitakavyotufikia.
HABARI KWA HISANI YA KIVIS-BLOG

Friday, January 27, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA JENGO JIPYA LA UBALOZI WA INDIA JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam mbele ya Balozi wa India Bw. Sandeep Arya .

 Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan picha mbali mbali zenye kuonyesha historia ya urafiki baina ya Tanzania na India wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi wa India jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert  jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya akihutubia wakati wa uzinduzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa nchini.

 Vikundi vya Utamaduni wa Kihindi vikionyesha uwezo wa kuzicheza ngoma za asili.


                 .............................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili wake wa miradi ya maji katika miji 17 nchi ambayo inalenga kupunguza tatizo la maji kwa wananchi wengi nchini.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 68 ya Siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya India sherehe ambazo zimeambatana na Uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi mpya ya Ubalozi wa India hapa nchini.


Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ufadhili wa miradi ya Maji pamoja na miradi mingine unaofanywa na Serikali ya India kwa Tanzania Bara na Zanzibar unadhihirisha wazi mahusiano mazuri yaliyopo yaliyoasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mahatma Gandhi wa India.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa India ni moja ya washirika muhimu katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo na Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu katika maeneo mengi ikiwemo ya kikanda na kimataifa kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na India.

Amesema kwa miaka mingi sasa mahusiano ya kindugu yamekuwa yaakiimarika katika sekta mbalimbali ikiwemo kisiasa,kidiplomasia,kibiashara, masuala ulinzi, utamaduni na mwingiliano wa watu na watu. 


Makamu wa Rais pia ameishukuru Serikali ya India kwa msaada wake wa shilingi milioni 500 alioutoa kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera ambao walikubwa na tetemeko la ardhi mwaka jana.

Ameeleza kuwa Mahusiano kati ya India na Tanzania yamekuwa na manufaa makubwa ambapo idadi kubwa ya watanzania wanaenda kupata mafunzo mbalimbali nchini India hasa Madaktari na wamekuwa msaada mkubwa katika kuokoa maisha ya Watanzania.



Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hotuba yake alitoa salamu za rambirambi kwa Serikali ya India kufuatia ajali ya treni iliyotokea katika Jimbo la Andhra Pradesh na kusababisha vifo vya watu 30 na kujeruhi wengine.

“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kutoka salamu za Pole kwa familia za wafiwa na majeruhi katika kipindi hiki kigumu kwa kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi na tunawaombea majeruhi wapone haraka. ’’
Kwa upande wake, Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya amemhakikishia Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Serikali ya India itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili.

RC MAKONDA AKUTANA NA MADEREVA TAX


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza  na Umoja wa Madereva Tax na kusikiliza kero zao, ,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Tax Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Ashiru akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akitoa elimu kwa madereva wa Madereva Tax leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda amekutana  na Umoja wa Madereva Tax Wilaya ya Ilala ilikusikiliza  kero zao zinazowakabili katika kazi yao.

Makonda ameyasema hayo leo alipokutana na madereva hao, amesema kunahitaji madereva wa tax kuwa mfumo bora wa kusaidia jiji la Dar es Salaam kuwa na huduma bora ya usafiri wa tax na wenye usalama

Amesema ni vyema kukawepo kifaa maalum kitakachoonesha umbali wa mteja anapokwenda ili alipe kulingana na umbali huo na ajue bei hiyo kuliko kukadiriana, pia amesema katika kufanikisha hayo serikali yake itaziondoa Tax bubu zote, na utaratibu wa kuweka rangi na namba kwenye magari utarudi ili Tax zote zitambulike.

Aidha amesema madereva wa tax kutoa taarifa za matukio ya kiharifu pale wanapohisi abiria waliyempakia ni mtu wa kufanya matukio ya kialifu.
 Makonda amesema wakitoa taarifa za uhalifu watalisaidia Taifa kuwa katika hali ya usalama, huku akiwataka ndani ya wiki moja wakae wajadiliane waje na mapendekezo yatakayokuwa na tija kwa pande zote.

Makamu Mwenyekiti wa Madereva  mkoa wa Dar es Salaam, Jacob Anyandwile amesema madereva hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozwa kodi kubwa na Mamlaka ya mapato nchini (TRA) pamoja na uwepo wa huduma ya Tax kwa njia ya mtandao unafanywa na kampuni ya UBA ambayo  imechangia kuharibu  soko ya usafiri huo.
Amesema kampuni ya UBA inatoza bei ndogo zaidi, pia gharama za uendeshaji hazilingani wanajikuta wao wanalipa kodi kubwa zaidi kuliko kampuni hiyo.

Katibu Mkuu wa Umoja huo Ramadhani Ashiru ameeleza kuwa kampuni hiyo ya UBA inatumia Tax bubu ambazo hazitambuliki kisheria.

Tuesday, January 24, 2017

MAMA JANETH MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKE WA RAIS WA UTURUKI


 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakikata utepe kuzindua jengo la zamani la King George’s V lililopo katika Jengo la makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam lililokarabatiwa na Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA).
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakitembelea maeneo mbalimbali ya historia ndani ya Jengo la makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam
 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akiongea na wageni alipotembelea ofisi za Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) zilizopo Masaki Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimshukuru Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan baada ya kumkabidhi viti maalum kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiojiweza(WHEELCHAIR).
  Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akikabidhi Mashine za kupumulia na kukua kwa watoto walizaliwa kabla ya muda (Njiti) Katikati ni Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli  na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru, Katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA).
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakikata utepe kufungua Ofisi za Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) zilizopo Masaki Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi za Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) zilizopo Masaki Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akiwa amekaa katika kiti cha kabila la kigogo alipotembelea katika kijiji cha Makumbusho Kijitonyama Jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akitoka katika moja ya nyumba ya kabila la kigogo alipotembelea katika kijiji cha Makumbusho Kijitonyama Jijini Dar es salaam.
 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akimueleza jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan Ofisini Kwake Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakifurahi na kinamama waliowalaki wakati anawasili ofisini kwa Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan baada ya kusaini kitabu cha wageni Ofisini Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan.

  Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akiongea na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo amemuahidi kuendelea kushirikiana katika kuwasaidia watoto na wanawake.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimshukuru Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan kwa kufanya ziara nchini pamoja na makubaliano ya kushirikiana katika kuiendeleza jamii Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

Monday, January 23, 2017

WAZIRI KAIRUKI AZINDUA AWAMU YA KWANZA YA OFISI YAKE KUHAMIA DODOMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakielekea Dodoma kwenye makao makuu ya nchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu wa Ofisi hiyo Bi. Susan Mlawi wakifuatilia kwa makini uamishwaji wa vifaa vya Ofisi yao kabala ya kuondoka kwenda Dodoma leo hii. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki amezindua rasmi safari ya awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Kairuki alisema umefika wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari ya kuamia makao makuu Dodoma ili kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.

“Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi Septemba 2016,Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii ya serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”,Aliongeza Mhe. Kairuki.

Amesema katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.

Katika hatua nyingine Mh. Kairuki alisema wale wote wanaohitaji kukutana na Waziri,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi zilizopo Dodoma na kwa masuala yote yanayohusuu Sera na Sheria za Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma kwa Ujumla yatatekelezwa Mjini Dodoma lakini.

Aidha masuala ya Mishahara,Uendelezaji rasilimali watu,Ukuzaji maadili,Anuai za jamii,Uchambuzi ushauri na Utendaji kazi na Huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano yataendelea kushughulikiwa na ofisi ya Dar es Salaam.

Alisema Ofisi yake itafunguliwa Rasmi Mjini Dodoma Tarehe 30 Januari 2017 na itakuwa katika Jengo la College of Humanities and Social Sciences katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma kama makao yake ya muda mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo.

OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA YAHAMIA DODOMA RASMI LEO

NITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KULETA MAENDELEO-KUMBILAMOTO

Naibu Meya wa Manispa aya Ilala, Omary Kumbilamoto, akikabidhi jezi kwa kikundi cha Makazi Kazi kilichopo katika mtaa wa Kaza Buti
 
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala akizungumza na Wananchi wa eneo la mtaa wa Kaza Butu katika kata ya Vingunguti.

 
Mwenyekiti wa Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mohamed Mluya, Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mjumbe wa Chama cha Wananchi (CUF) Salma Emmanuel, Akizungumza juu ya mambo yake yaliyotekelezwa na Diwanihuyo
Mwenyekiti wa Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mohamed Mluya, akikabidhi jezi kwa vikundi vya Joging
Naibu Meya na wenzie wakicheza muziki mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
Wananchi wakifatilia mkutano huo kwa makini
Baadhi ya vijana wa mtaa wa kaza buti wakifatilia kwa makini mkutano huo unavyoendelea
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mtambani ,Sharifu Abdalah akikabidhi jezi kwa kikundi cha Joging
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala akisalimiana na wazee maharufu mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wananchi wa mtaa wa Kaza buti
Dj akifanya yake katika mkutano huo.

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii 


Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vinguti , Omary Kumbilamoto, ameahidi kuendelea kushirikiana na wakazi wa kata hiyo hili kuakikisha wanapata maendeleo. 

Kumbilamoto amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa mtaa wa Kaza buti kata ya Vingunguti wakati akikabidhi vifaa vya michezo na mabati kwa tasisi ya Makazi kazi na vikundi vya michezo. 

“nitoe shukrani kwa wakazi wa eneo la kazabuti kwa jinsi mlivyoweza kuniamini katika uchaguzi mkuu mwaka jana na kunipa fursa ya kuwa Diwani wenu na leo nimekuja kuwatembelea kwa ajili ya kutimiza moja ya ahadi zangu hivyo naomba niwaambie kuwa nitakuwa nanyi bega kwa bega katika kuakikisha kuwa tunaleta maendeleo katika kata yetu” amesema Kumbilamoto. 

Kumbilamoto amesema kuwa amemaliza mwaka mmoja ndani ya utawala wake kwa kuweza kutimiza ahadi kadhaa ambazo aliahidi ikiwemo ununuzi gari ya kubebea wagonjwa , Mashine yakufulia katika Zahanati ya vingunguti na ujenzi wa choo kwa ajili ya wodi ya kinamama wajawazito. Aidha ametaja kuwa pia katika mwaka huu mmoja maeweza kuwasaidia wanawake wajasilimali ambao aliwapa vyerehani viwili hiki kuendeleza vikundi vyao. 

Kumbilamoto alimaliza kwa kuwataka wakazi wa Vingunguti kuwa wachapakazi kwa kila jambo kama Rais wanchi Dkt John Pombe Magufuli.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...