Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na Alhaji Sheidu Bello Ozigis ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Nigeria ( Permanent Secretary for the Ministry of Tourisim, Culture and National Orientation) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Abuja, March 8, 2010 kuhudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa nchi kuhusu maendeleo ya Biashara na viwanda ya kilimo barani Afrika uatakaofanyika Abuja March 10, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Tuesday, March 09, 2010
Waziri MKuu Abuja
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na Alhaji Sheidu Bello Ozigis ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Utamaduni wa Nigeria ( Permanent Secretary for the Ministry of Tourisim, Culture and National Orientation) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Abuja, March 8, 2010 kuhudhuria mkutano wa viongozi wakuu wa nchi kuhusu maendeleo ya Biashara na viwanda ya kilimo barani Afrika uatakaofanyika Abuja March 10, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Monday, March 08, 2010
Kakobe asalimu amri


Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF),Zacharia Kakobe akizungumza na wanahabari kanisani kwake kuhusu kuridhia kupitishwa kwa nyaya za umeme zenye msongo mkubwa mbele ya eneo la kanisa lake jijini Dar es Salaam jana.Picha na Venance Nestory.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe sasa amekubali Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupita umeme wa msongo mkubwa mbele ya kanisa lake huku akiendelea kushikilia msimamo kwamba uamuzi uliofanywa na serikali wa kuhalalisha njia hiyo bado siyo sahihi.
Hakuishia hapo bali amekuja na shutma nyingine dhidi ya serikali akisema kwamba shauri hilo limemfumbua macho na kubaini kwamba baadhi ya watendaji wa serikali wana agenda za siri za kuhujumu Ukristo nchini hivyo ameamua kubadili mbinu za mapambano dhidi yao.
Askofu Kakobe aliyasema hayo jana ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kutoa tamko la serikali la kupuuzia mbali madai ya waumini wa kanisa hilo kwamba kanuni za kitaalamu za kuzuia wasidhurike na njia hiyo ya umeme wa kilovoti 132, haukuzingatiwa.
“Sasa hivi hatuna kipingamizi chochote, waje waendelee na kazi yao,” alisema Kakobe ambaye Desemba mwaka jana alitangaza eneo hilo kuwa ni la hatari kwa wafanyakazi wa Tanesco na tangu wakati huo likawa linalindwa na waumini wa kanisa hilo waliovalia fulana za njano zenye maandishi “Tanesco mwogopeni Mungu.”
Pamoja na kuridhia Tanesco waendelee na mradi huo, Askofu Kakobe alisisitiza kwamba kwenye uamuzi huo haki ilifinyangwa na uamuzi wa kibabe uliochochewa na mambo ya udini, lakini akasema sasa amebadili mbinu na mikakati ya kukabiliana nao.
Akionekana kuzungumza kwa utaratibu na uangalifu mkubwa, alitaja miongoni mwa mbinu zake za sasa kuwa ni kuwasiliana na makanisa mengine ya Kikristo nchini kutaka wajadili hujuma dhidi yao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Miongoni mwa hujuma hizo alidai kwamba ni baadhi ya waumini wa kanisa lake kuanza kubaguliwa kwenye maeneo ya kazi, jambo ambalo alilielezea kuwa “ni la hatari na linaotesha mbegu ya ubaguzi wa udini jambo ambalo ni kinyume na Katiba ya nchi.”
“Hili siyo siri limefanyika. Muumini wetu aliyekuwa anafanya kazi wizara ya nishati aliitwa na kuulizwa anasali wapi na ilipobainika ni muumini wa kanisa hili, kwa muda mfupi tu akakabidhiwa barua ya uhamisho. Huu ni ubaguzi.”
Sunday, March 07, 2010
Siku ya Wanawake ya Zain
Dua ya pamoja kuwaswalia wazee
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein kulia, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Salmin Amour wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma katikati, Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakisoma Dua ya pamoja kwenye eneo la Makaburi ya Wazee baada ya kumaliza kusoma Hitima maalum iliyoambatana na Maulid yanayosomwa kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Uguja jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein wa pili kulia, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha kulia, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salmin Amour katikati, na Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, wakisoma Hitima maalum ya kuwaombea Wazee mbalimbali waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika jana katika msikiti wa kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa pili kulia, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi wa kwanza kushoto, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour wa pili kushoto na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, wakisoma Dua ya pamoja baada ya kumalizika Dhifa maalum ya Maulid ilioyoandaliwa na Dk. Salimin Amour, inayofanyika kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja jana.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa kwanza kushoto, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Salmin Amour wa pili kushoto, Rais mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi wa pili kulia, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma, wakielekea kwenye eneo la Makaburi ya Wazee walitangulia mbele ya Haki mara baada ya kusoma Hitima maalum kwa ajili ya Marehemu hao katika Msikiti Mkuu wa kijiji cha Kidombo uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja jana, ambapo Dua hiyo iliambatana na Maulidi ya nayayosomwa kila mwaka kijijini hapo. Amour Nassor (VPO)
Friday, March 05, 2010
Uzinduzi mahakama ya Rufani




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Jaji Mkuu wa Tanzania Augustine Ramadhan pamoja na familia za majaji kabla ya kuzidua jengo la kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa Kwanza Mzalendo, Hayati Augustine Said kwenye mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam . Kwenye picha yupo pia mke wa Jaji Saidi Bi Helena, jengo lenyewe waoza kuliona pia waweza kuona sanamu la jaji Saidi lililowekwa kama kumbukumbu yake. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Thursday, March 04, 2010
Zantel Waja Na "Ofa Ya Simu Za Gumzo"

Mkuu wa Huduma na Bidhaa wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel Bw. Brian Karokola (kushoto) akitoa ufafanuzi wa Ofa mpya ya huduma ya simu za mkononi na mezani kwa gharama nafuu iitwayo “Ofa ya simu za Gumzo”, kwa lengo la kupunguza gharama za kupiga simu kwa wafanyabiashara wadogowadogo na matumizi ya nyumbani . Kulia ni Meneja masoko wa kampuni hiyo Bw. William Mpinga.
BREKING NYUUUUUUZZZZZ:NEHEMIA MCHECHU AULA NATIONAL HOUSING

Nehemia Kyando Mchechu- Bosi Mkuu Shirika la Nyumba Tanzania [NHC]
Kwa mujibu wa kifungu Na. 18 (1) cha Sheria Na. 2 ya 1990, iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (The National Housing Corporation Act No. 2 of 1990) Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amemteua Ndugu Nehemia Mchechu (37) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Uteuzi huu unaanzia tarehe 1/3/2010.
Kabla ya uteuzi huu Ndugu Nehemia Mchechu alikuwa Mkurugenzi
Mkuu (Chief Executive Officer) wa Benki ya “Commercial Bank of Africa”.
Chini ya Uongozi wake benki hiyo imepata mafanikio makubwa sana hapa nchini, na ni moja kati ya benki tano zilizoanza utaratibu wa kutoa mikopo ya nyumba kwa Watanzania.
Ndugu Nehemia Mchechu akishirikiana na Bodi mpya ya Shirika hili na timu ya Menejimenti ya Shirika hili, amepewa jukumu la kulifanyia mageuzi makubwa Shirika hili ili liingie katika biashara kubwa ya kujenga nyumba katika Mikoa yote na kuziuza kwa mikopo kwa watanzania wa kipato cha chini na kati, ambalo ndilo lengo kuu la Shirika hili tangu lilipoanzishwa mara tu baada ya Tanganyika kupata Uhuru Desemba 9, 1961.
Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria Na. 2 ya 1990 iliyounda Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Bwana K. Masudi Issa Msita kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo. Bwana K. Masudi Issa Msita ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Ujenzi (National Construction Council).
Wakati huo huo, na kwa mujibu wa Sheria hiyo hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo.
1. Msajili wa Hazina - (Wizara ya Fedha).
2. Mkurugenzi wa Nyumba - (Wizara ya Ardhi).
3. Prof. W.J. Kombe - (Chuo Kikuu cha Ardhi).
4. Bwana Enock Maganga - (Benki Kuu).
5. Bi Subira Mchumo - (Sekta Binafsi).
6. Bwana Elius Mwakalinga - (Wizara ya Miundombinu).
7. Bi. Shally Raymond - (Mbunge)
Uteuzi huu unaanza tarehe 28/02/2010 na ni wa miaka mitatu.
Imetolewa na:-
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi
Subscribe to:
Posts (Atom)
MKUTANO WA CATA UANGAZIE MIJADALA YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO - MAKAMO WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema matumizi ya mifumo ya kisasa ya teknolojia ni chachu kati...
-
Hapa mmoja wa watoto hao akiwa na kijana mwenzake mwenye miaka 18, wote wako sawa lakini yeye hawezi kuzungumza kama watu wa kawaida. Mama S...
-
Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo kati...
-
Mdau Julius Samwel hivi karibuni alikuwa huko Mwanza na hizi ndizo alizofanikiwa kutumegea, wadau hebu someni hicho kibao mniambie kuna nini...