Friday, October 30, 2026

RAIS SAMIA NA RAIS WA ANGOLA WAWASILI KWA RELI YA SGR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiambatana na mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço, wamewasili jijini Dodoma, Oktoba 30, 2026 wakitokea Dar es Salaam kwa kutumia reli ya kisasa ya SGR.

Viongozi hao wamewasili Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais wa Angola nchini Tanzania, yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kukuza ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali.

Safari hiyo ya kihistoria kwa Mhe. Rais Lourenço kutumia Reli ya SGR, imeonesha umuhimu wa matumizi ya miundombinu ya kisasa ya usafiri wa reli nchini Tanzania, huku viongozi hao wakiendelea na ratiba ya ziara hiyo jijini Dodoma ikiwemo uzinduzi rasmi wa Mji wa Serikali uliopo Mtumba jijini humo.







No comments: