Thursday, October 29, 2026

CHUO KIKUUU MZUMBE YAWATAKA WAHITIMU KUTENGENEZA AJIRA BADALA YA KUTEGEMEA KUAJIRIWA



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha a
kizungumza leo, Oktoba 29, 2026, jijini Dar es Salaam, katika Mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu Mzumbe, aliyofanyika katika Ukumbi wa 

 Chasisitiza matumizi ya Akili Mnemba (AI), ubunifu na maarifa kukabiliana na changamoto za jamii.

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

Chuo Kikuu Mzumbe kimewataka wahitimu wake kutumia elimu, ubunifu na teknolojia ya kisasa kujitengenezea fursa za kiuchumi na kuzalisha ajira kwa wengine, badala ya kutegemea kuajiriwa pekee.

Wito huo umetolewa leo, Oktoba 29, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa Mahafali ya 25 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam, yaliyohudhuriwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Akizungumza katika mahafali hayo, Dkt. Shein amewapongeza wahitimu kwa juhudi, nidhamu na uvumilivu waliouonesha katika safari yao ya kitaaluma, huku akiwakumbusha kuwa thamani ya elimu waliyoipata inapaswa kuonekana kupitia mchango wao katika maendeleo ya jamii na Taifa.

Amesisitiza umuhimu wa uadilifu, nidhamu, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora katika utekelezaji wa majukumu yao, akieleza kuwa sifa hizo ni msingi muhimu wa mafanikio katika maisha na utumishi.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amesema mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya soko la ajira yanawataka wahitimu kuendelea kujifunza na kuongeza ujuzi hata baada ya kumaliza masomo yao.

Amesema matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususan Akili Mnemba (AI), yanafungua fursa mpya za kuongeza ufanisi, kuchochea ubunifu na kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazokabili jamii.

Prof. Mwegoha ameeleza kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kinaendelea kuboresha programu zake za masomo ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira na vipaumbele vya maendeleo ya Taifa, sambamba na kutoa mafunzo na huduma za ushauri wa kitaalamu.

Ameongeza kuwa wahitimu wanapaswa kutumia maarifa na teknolojia kwa manufaa ya jamii na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Balozi Modest Jonathan Mero, amewahimiza wahitimu kutambua kuwa elimu ya chuo kikuu si tiketi ya kupata ajira pekee, bali pia ni nyenzo ya kujiajiri, kubuni fursa na kuwawezesha wengine kiuchumi.

Amesisitiza umuhimu wa nidhamu na matumizi sahihi ya elimu katika maeneo mbalimbali ya kazi na shughuli za uzalishaji.

Akizungumza kwa niaba ya wahitimu, Mhitimu Bora wa Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam, kwa mwaka 2026, Enoishi Kimirei, ametoa shukrani kwa viongozi wa chuo, wahadhiri, watumishi, wazazi na walezi kwa mchango wao katika kufanikisha safari yao ya kitaaluma.

Mahafali hayo yameweka msisitizo katika umuhimu wa elimu inayozalisha matokeo, matumizi ya teknolojia na maandalizi ya wahitimu wenye uwezo wa kushindana katika soko la ajira, kujiajiri na kuchangia maendeleo ya Taifa.

No comments:

CHUO KIKUUU MZUMBE YAWATAKA WAHITIMU KUTENGENEZA AJIRA BADALA YA KUTEGEMEA KUAJIRIWA

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha a kizungumza leo, Oktoba 29, 2026, jijini Dar es Salaam, katika Mahafali ya 25 ya Ch...