Wednesday, October 28, 2026

MAKAMU WA RAIS NDEJEMBI AMFARIJI IGP WAMBURA KUFUATIA KIFO CHA BABA YAKE


Dar es Salaam, Oktoba 28, 2026.

Katika kuonesha upendo, utu na mshikamano wakati wa majonzi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amemtembelea na kumpa pole Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kufuatia kifo cha baba yake mzazi, marehemu Deusdedit Mwita Wambura.

Makamu wa Rais amefika katika makazi ya IGP Wambura, Masaki jijini Dar es Salaam, na kuungana na familia hiyo katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao, aliyefariki dunia Oktoba 24, 2026.

Ziara hiyo ni ishara ya upendo na mshikamano wa kibinadamu, ikikumbusha umuhimu wa kusimama pamoja, kufarijiana na kutiana moyo wakati wa misiba, bila kujali nafasi au majukumu aliyonayo mtu katika jamii.

Katika nyakati za majonzi, uwepo wa wanaotujali huwa faraja kubwa kuliko maneno.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Deusdedit Mwita Wambura mahali pema peponi na aijalie familia yake nguvu, subira na moyo wa ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.





No comments:

WAZIRI WA ARDHI ZANZIBAR, KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI NA ZHC WAIPONGEZA NHC KWA MIRADI YA KISASA YA KAWE

Mkurugenzi Mkuu Hamad Abdallah akiwapokea wajumbe kutoka Zanzibar. Mkurugenzi Mkuu Hamad Abdallah akitoa wasilisho kuhusu shughuli, mafaniki...