Tuesday, September 29, 2026

Uwanja wa Ndege wa Kisasa Mikumi Kukamilika Novemba

Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Katika kufungua miundombinu zaidi ya utalii nchini, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, inakamilisha uwanja mwingine wa ndege wa kisasa utakaoleta mageuzi katika sekta ya utalii nchini.

Uwanja huo unaojengwa katika Hifadhi ya Taifa Mikumi, lango muhimu la utalii unaounganisha Bara na Zanzibar, una urefu wa kilometa 1.8 na ukiwa na majengo ya kisasa ya kupokea na kuondokea abiria, jengo la zimamoto na kituo maalum cha hali ya hewa, unatumia teknolojia ya kisasa ya lami maalum (polymer) inayounda tabaka gumu linalodumu kwa zaidi ya miaka 15.

“Tulipopokea taarifa ya maandishi pale Wizarani mlionesha Novemba mwaka huu mradi huu muhimu utakamilika. Hakika nimefika hapa leo na nimejionea kazi nzuri mliyoifanya na nimejiridhisha kuwa kweli Novemba 15, 2026 mradi huu wote mtakuwa mmetukabidhi,” anasema Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, alipokagua mradi huo leo Septemba 29, 2026, Hifadhini Mikumi. 

Viwanja vingine vitatu kama hivyo vimekamilika ikiwemo Hifadhi ya Nyerere (1) na Hifadhi ya Ruaha (2).







No comments:

Uwanja wa Ndege wa Kisasa Mikumi Kukamilika Novemba

Na Mwandishi Wetu, Morogoro  Katika kufungua miundombinu zaidi ya utalii nchini, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu ...