Sunday, September 20, 2026

DKT. MWIGULU AWASILI ROMA, ITALIA KUIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA ONE HEALTH







Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Roma, Italia, leo Septemba 20, 2026, kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja katika Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health in Agrifood Systems).

Mkutano huo wa siku tatu, unaotarajiwa kufanyika Septemba 21–23, 2026 katika Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), utawakutanisha viongozi, wataalamu na wadau kutoka mataifa mbalimbali kujadili hatua za pamoja za kuimarisha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira kupitia mifumo endelevu ya chakula na kilimo.

Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Leonardo da Vinci (Fiumicino), Dkt. Mwigulu amepokelewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo unatoa fursa ya kushiriki mijadala ya kimataifa kuhusu usalama wa chakula, kilimo endelevu, afya ya mimea na wanyama, mabadiliko ya tabianchi, usugu wa vimelea dhidi ya dawa pamoja na namna ya kuimarisha mifumo ya chakula na kilimo inayostahimili changamoto mbalimbali.

Mkutano huo pia unalenga kuimarisha ushirikiano baina ya sekta na mataifa katika kutekeleza dhana ya “Afya Moja”, inayotambua kuwa afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira ina uhusiano wa karibu na inahitaji hatua zinazoratibiwa kwa pamoja.

 

No comments:

DKT. MWIGULU AWASILI ROMA, ITALIA KUIWAKILISHA TANZANIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA ONE HEALTH

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Roma, Italia, leo Septemba 20, 2026, kumwakilisha Rai...