Mkurugenzi
Mtendaji wa NIC Insurance Kaimu Mkeyenge Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa Kampeni ya NIC Kitaa iliyofanyika Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
*Yazindua Kampeni ya NIC Kitaa ,wenye madai wafike katika kampeni kulipwa kiganjani mwao
Na Chalila Kibuda,Michuzi Blog
NIC
Insurance imesema kuwa ina kazi na wajibu wa kutoa elimu ya uelewa bima
nchini ikiwa utekelezaji maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita ya
Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Kampeni ya NIC Kitaa Mkurugenzi Mtendaji wa NIC
Insurance Kaimu Mkeyenge amesema kuwa kampeni hiyo itakwenda nchi nzima
katika kutoa elimu ya uelewa wa bima.
Amesema
kuwa takwimu ya wananchi wa Tanzania wenye uelewa wa kuhusu bima ni
asilimia mbili hivyo kazi lengo ni kufikia asilimia tano.
Amesema
NIC Kitaa amesema lengo ni kutoa elimu ya bima kwa watanzania waelewe
faida na muhimu katika kulinda uwekezaji wa biashara na mali zao.
Amesema
wanaingia msimu wa pili wa kampeni wa NIC Kitaa kusogeza huduma kwa
wananchi na kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wote na kutambua
umuhimu wa bima.
"Uelewa
wa bima bado uko chini sisi kama Taasisi kongwe yenye msuli mkubwa
katika mtaji tunawajibu wa kusaidia serikali kwa sababu bima ni
ukusanyaji wa fedha za wananchi ambao wanahisi wakipata majanga
wasaidiwe na faida yake inaweza kusaidia uchumi ambao unawekezwa katika
taasisi za fedha zikiwemo benki"amesema Mkeyenge
Amesema katika mikakati ya kutoa uelewa wa bima wanakwenda kuongeza mtaji kwenye soko hususan sekta ya bima.
Mkeyenge
amesema kutoa elimu hiyo ni kuendeleza sera ya Rais Dk. Samia Suluhu
Hassan ya bima kwa wote na kuhakikisha watanzania wote wanatumia bima.
Aidha
aliongeza kuwa kuwa pamoja na kutoa elimu ya kampeni hiyo
wataambatisha na kuandikisha bima kwa wateja wapya na kulipa madeni sio
lazima waje ofisini wamewasogezea huduma haduma hapo.
Kampeni hiyo itafanyika nchi nzima kwa sasa wameanza na mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Singida.
Comments