Vodacom Tanzania na Benki ya TCB wameujulisha umma na wateja wao kwamba ujumbe wa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii unaodai kwamba huduma ya M-Koba inakaribia kufungiwa kutokana na madai ya madeni yasiolipwa kwa Serikali ni wa uongo na uzushi unaokusudia kuleta taharuki kwenye jamii.
Katika
taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Vodacom na Benki ya TCB
wawahakikishia wateja wao wote wa M-Koba kwamba akaunti zao ziko salama
na zinafanya kazi kama kawaida.
Vodacom
na Benki ya TCB pia wamewahakikishia wateja wa M-Koba kwamba usalama wa
wateja na usalama wa akaunti zao ni kipaumbele chake cha juu na
wanatumia njia madhubuti za kulinda faragha ya wateja na kudumisha
uaminifu wa huduma zao za kifedha
Umma
unashauriwa kupuuza habari za uongo na kutegemea njia rasmi za Vodacom
kwa taarifa za uhakika. Vodacom pia inafanya kazi kwa karibu na mamlaka
husika ili kubaini chanzo cha habari hizi za uongo na kuchukua hatua
zinazostahili.
Huduma
ya M-Koba inaletwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya TCB
chini ya usimamizi wa Benki kuu ya Tanzania (BOT).
Comments