Thursday, January 31, 2019

MKURUGENZI WA JIJI AAINISHA MAENEO YA UWEKEZAJI KWA NHC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani leo amekutana na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi na kujadiliana maeneo mbalimbali ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili yakiwemo ya uwekezaji katika maeneo ya kimkakati jijini humo.  Mkurugenzi huyo ameeleza imani yake kubwa kwa Shirika na akahimiza NHC iwekeze zaidi katika ujenzi wa majengo ya kati na ya juu.
 Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akikaribishwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani akiendelea na mjadala na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi.

SPIKA NDUGAI AKUNWA NA UTENDAJI WA NHC AAGIZA KASI IONGEZWE

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani leo amekutana na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mheshimiwa Job Ndugai na kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo.  Spika Ndugai ameeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji miradi inayofanywa na Shirika na akahimiza kasi hiyo iongezwe ili kuwapatia Watanzania wengi zaidi huduma ya nyumba hususani wale wa Dodoma yalipo makao makuu ya nchi.
Spika akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu, Dk Banyani.
 Dk.  Banyani akitoka nje ya jengo la bunge baada ya kukutana na Spika Ndugai.
 Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mheshimiwa Job Ndugai akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu Dk Banyani (wa pili kulia) baada ya mkutano huo.
Spika Ndugai akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.

 Mjadala ukiendelea baina ya pande mbili hizo.

 Wakifurahia jambo baada ya majadiliano ya hoja kadhaa za maendeleo ya sekta ya ujenzi na Shirika kwa ujumla.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Yahya Charahani akizungumza jambo mbele ya Spika Ndugai.
  
Mjadala ukiendelea na Spika Mheshimiwa Job Ndugai wakati wa mkutano huo.

 Mkurugenzi Mkuu wa NHC,  Dk.  Banyani (wa Kwanza Kulia) akitoka nje ya jengo la bunge baada ya kukutana na Spika Ndugai. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo na Masoko, Itandula Gambalagi (wa kwanza kushoto) na katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.

MKURUGENZI MKUU ATEMBELEA ENEO JIPYA KUNAKOKUSUDIWA KUJENGWA MAKAZI YA WATUMISHI WAANDAMIZI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk Maulidi Banyani jana alitembelea eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu.  Eneo lipo karibu kabisa na ulipo mji wa Serikali kulikojengwa wizara mbalimbali za Serikali. Pichani Afisa Miliki wa NHC Dodoma Jaffari Chege akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu mfano wa michoro ya eneo hilo. 
 Ukamilishaji wa ujenzi wa mji wa kiserikali ukiendelea ndani ya jengo la Wizara ya Fedha wakiwa wanafanya skimming.
 Jengo la Wizara ya Fedha lilivyo sasa.

Eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu.
 Kaimu Mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa Abdallah Migilla akiteta jambo na Injinia Hassan Mohammed wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye eneo kunakojendwa wizara ya Viwanda na Uwekezaji.
 Mkurugenzi Mkuu akitembelea eneo la wizara hizo

 Mkurugenzi Mkuu akielekeza jambo.

 Eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu.

Umaliziaji ukiendelea katika wizara ya Viwanda na Uwekezaji 

Monday, January 28, 2019

NAIBU WAZIRI DK MABULA AICHAGIZA NHC KATIKA UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA

Mhandisi Peter Mwaisabula ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula aliyetembelea mradi huo wa ujenzi leo asubuhi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula akitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Fedha na Mipango linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma, Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula akielekea kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Viwanda na Uwekezaji linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma,
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio  akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula aliyetembelea mradi huo wa ujenzi leo asubuhi,



Mhandisi wa Matengenezo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Julius Ntoga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela kwenye mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango lililopo eneo la Mtumba jijini Dodoma.


Mhandisi Peter Mwaisabula ambaye anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma akimsindikiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela  aliyetembelea mradi huo wa ujenzi leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akisalimiana na mmoja wa waratibu wa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akati alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Fedha na Mipango linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani (Kushoto)
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani mbele ya mradi wa jengo la Nishati.
Jengo la Wizara ya Viwanda na Biashara likiwa katika hatua za mwiszho za ujenzi.



Jengo la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi likiwa limeshaanza kuwekwa madirisha na kenzhi kwaajili ya kuanza kuezeka linavyoonekana kwa sasa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Pius Tesha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akiangalia ramani ya jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa. Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akiangalia ramani ya jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa. Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Udhibiti wa. Huduma za Nishati na Maji (EWURA) likiwa limeanza kuinuka kuelekea ghorofa ya kwanza.
Mmoja wa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa Ewura, Hassan Bendera akiwaelekeza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Sophia Kongela  na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani,
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula ameendelea kufurahishwa na maendeleo mapya na hatua zinazopigwa kila kukicha katika ujenzi wa ofisi za wizara katika mji wa serikali ya Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Dk Mabula alitoa kauli hiyo leo tarehe 28 Januari 2019 wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi za Serikali katika mji wa Mtumba mkoani Dodoma unaojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo liko chini ya Wizara yake.
Alisema kazi inayofanywa na shirika la Nyumba la Taifa kujenga ofisi za Serikali katika mji huo kwa sasa unaenda kwa kasi na unatia moyo kwani kila kukicha kila mhandisi anayesimamia mradi anakuwa anafanya ubinifu wake ambao ni tofaujti na wamwingine na hivyo kuchagiza maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo.
Katika mradi huo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kampuni yake ya ujenzi inajenga ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Nishati pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, Dk Mabula amefurahishwa na ufuatialiaji wa ujenzi wa ofisi hizo unaofanywa na Wizara ya Fedha pamoja na Viwanda na Biashara na kueleza kuwa hatua hiyo inalifanya Shirika hilo kufanya kazi kulingana na mahitaji ya wateja wake.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...