Friday, December 21, 2018

SHIRIKA LAANZA KUFUNGUA NJIA KWENYE MAENEO YANAYOPIMWA KWAAJILI YA MAKAZI CHATO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitoa maelekezo kwa Afisa Upimaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Denis Mtafya wakati alipotembelea eneo la Rubambangwe linalopimwa na Shirika la Taifa na kuanza kuuzwa kwa wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Chato,  Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon akijadiliana jambo na ujumbe kutoka Shirika la Nyumba la Taifakuhusu utekelezaji wa miradi ya upimaji viwanja na ule wa uchoraji ramani ya ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa wa michezo wa Chato.

                                     &&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk. Maulidi Banyani jana aliendelea na ziara katika miradi ya Chato apartments  na Chato affordable houses na kufanya kikao na Mkuu wa wilaya ya ChatoMhandisi Mtemi Msafiri Simeon na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Eliud Leonard Mwaiteleke kuhusu miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa wilayani humo na ile iliyotekelezwa na kumueleza Mkuu wa Wilaya kuwa zoezi la kufungua barabara kwenda kwenye maeneo yanayopimwa..

Naye Mkuu wa wilaya ya Chato,  Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon aliwakaribisha ujumbe kutoka Shirika la Nyumba la Taifa na kuelezea fursa zilizopo Chato. 

Alisema kuwa Wilaya ya Chato kuna mapori ya kuvutia yakiwamo ya Burigi,  Biharamulo,  Kimisi,  Rubondo,  Rumanyika na uwanja wa ndege ambavyo vyote kwa ujumla vitaweza kuwavutia watalii wengi.

Mhandisi Msafiri alisema wao kama wilaya wanahitaji kujipanga kabla ya maendeleo kuja kuwazidi uwezo na anachokiomba ni Shirika kuendelea na upimaji wa viwanja katika eneo la Rubambangwe japo kwa awamu ya kwanza faida itakuwa ndogo. 

Dk. Banyani akizungumzia hilo alisema mradi huo ni wa kipaumbele na kwamba Shirika la Nyumba kwa sasa linajisogeza kwa wananchi kwa kuwasaidia kuwatafutia suluhu ya matatizo yao na kuwajengea nyumba bora.

Akizungumzia zoezi la kufungua barabara alisema  limeanza jana na linasimamiwa na NHC. 

Kuhusu suala la uwanja wa mpira wa Chato alisema Shirika limeandaa  concept ya uwanja huo na linaendelea kufanya tafiti sehemu mbalimbali ili kupata uwanja bora.

 Nyumba za makazi za gharama nafuu za Chato
 Nyumba za makazi za ghorofa za Chato

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akitoa maelekezo kwa Afisa Upimaji wa Shirika la Nyumba la Taifa, Denis Mtafya wakati alipotembelea eneo la Rubambangwe linalopimwa na Shirika la Taifa na kuanza kuuzwa kwa wananchi.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon baada ya kumaliza kikao Chato.
 Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu.
  Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato.
 Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato.

 Mkuu wa wilaya ya Chato,  Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon akijadiliana jambo na ujumbe kutoka Shirika la Nyumba la Taifakuhusu utekelezaji wa miradi ya upimaji viwanja na ule wa uchoraji ramani ya ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa wa michezo wa Chato.

 Kaimu Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara, William Genya akijadiliana jam Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Eliud Leonard Mwaiteleke jana wilayani Chato.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akikagua eneo wakati alipotembelea eneo la Rubambangwe linalopimwa na Shirika la Taifa na kuanza kuuzwa kwa wananchi.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Abdallah Migila akifuatilia mjadala.

 Mkurugenzi Mkuu akitafakari jambo wakat5i akikagua mradi wa upimaji viwanja wa Chato  jana.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani akikagua eneo wakati alipotembelea eneo la Rubambangwe wilayani Chato linalopimwa na Shirika la Taifa na kuanza kuuzwa kwa wananchi.

Mkurugenzi Mkuu akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chato wakati Mkurugenzi Mkuu alipofika kumsalimia Mkurugenzi huyo,

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...