Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili ya mwajiri bora wa mwaka 2018 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi katika
hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha
Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili ya
mwajiri bora wa mwaka 2018 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa
Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi katika
hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha
Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa
Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Godlove Godwin na Neema Msita katika
hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha
Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abeld Joram na Neema Msita katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abeld Joram na Neema Msita katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa na maafisa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Godlove Godwin na Neema Msita katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akikabidhi tuzo ya mshindi wa pili ya mwajiri bora wa mwaka 2018 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Tuzo mbili za mshindi wa pili za Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 za Mwajiri bora wa ndani na mwajiri bora katika sekta ya umma katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Omari Makalamangi akiwa ameshikilia tuzo ya mwajiri bora baada ya kuipokea kutoka katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba.
Mwakilishi
wa Tanzania Cigarette Company (TCC), akipokea Tuzo ya Mwajiri Bora wa
Mwaka 2018 baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi afasi ya tatu katika
hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa
Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama (MB).
Mwakilishi
wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Bi. Lilian Makau akipokea Tuzo ya
Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya Kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi
ya pili katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania
(ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni
rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).
Wafanyakazi
wa Geita Gold Mine (GGM) wakifurahiya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka
2018 pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) baada ya
kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya kwanza kwenye
hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa
Mlimani City, tarehe 14 Disemba 2018.
…………………………………………………………….
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),
Disemba 14 2018 kimeandaa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2018
zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Tangu
kuanzishwa kwake mwaka 2005, tuzo hizo zimejikita katika kutambua
waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa guvu kazi na rasilimali watu
kwa lengo la kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu na kupelekea
kukuza uzalishaji wa kibiashara.
Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau
mbali mbali wakiwemo Mh. Jenista Mhagama, Mh. Anthony Mavunde, Mhe.
Stella Ikupa, Mkuu wa Mkoa DSM, Mhe. Paul Makonda, Balozi wa Norway
nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark nchini, Bw. Einer H.
Jensen na Balozi wa China nchini Nd. Wang Fe, pamoja na taasisi mbali
mbali ikiwemo TUKTA na ILO.
Tuzo hizo zinazofanyika kila
mwaka zimasaidia kuhamasisha wanachama kuchukulia masuala ya ajira na
usimamizi wa rasilimali watu kama misingi muhimu katika kumwezesha
mwajiri kuwana wafanyakazi wenye uwezo na ueledi ili kukidhi mahitaji ya
ushindani katika biashara.
Sherehe ya utoaji tuzo
iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa
Mgeni Rasmi, zimekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara
hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati
kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya kufanya biashara nchini.
Tuzo hizo ambazo kwa mwaka 2017
ziliboreshwa kwa kuongezewa vipengele 12 vipya vya Hali nzuri kwa
Wafanyakazi (Employee Wellness), Kuvutia na kutunza wafanyakazi wenye
ujuzi (Attraction and Retention), Mahusiano Mazuri Mahali pa Kazi
(Industrial Relations), Kujali kazi na maisha nje ya Kazi (Work Life
Balance), Mwajiri anayekubalika na Kufahamika (Employer Branding),
Usimamizi wa Wafanyakazi kwa kuzingatia Umri (Managing an Aging
Workforce), Uwekezaji katika Teknolojia (Technology Investment), Tuzo
kwa ajili ya Sekta Binafsi (Private Sector Award), Tuzo kwa Sekta ya
Umma (Public Sector Award), Tuzo kwa Ajili ya Mashirika ya Kijamii (
Civil Society Award) na Tuzo ya Mwajiri Mzawa (Indigenous Employer
Award) , zitaendelea na vipengele hivyo vipya kwani vinatoa fursa kwa
wanachama kufanyia kazi vipengele hivyo kwa lengo la kuboresha mazingira
ya kazi na ajira kulingana na mahitaji ya waajiri nchini.
Akizumgumza na wageni waalikwa
Mgeni Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu alisema kwamba
serikali inatambua mchango wa waajiri kutoka sekta zote na itaendelea
kushirikiana nao pamoja na Vyama vya Wafanyakazi na wananchi kwa ujumla
katika kutimiza azma ya nchi yetu kujitegemea.
Mhe. Jenista Mhagama aliongeza
kuwa serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungazo wa
Tanzania, Dr. John Joseph Magufuli imebeba jukumu la kuboresha
miundombinu katika nyanja za usafirishaji wa anga, reli na maji, afya,
nishati, elimu na mawasiliano ambayo kwa kiasi kikubwa zinaongeza
uzalishaji wa nchi kupitia waajiri wa sekta binafsi na umma.
Aidha Mh. Mhagama alipongea Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa shughuli zake mbali
ikiwemo Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa
Uongozi kwa Mwaka2018, Mwanamke wa Wakati Ujao inayofanyika kwa
ushirikiano na Shirikisho la Vyama vya
Waajiri nchini Norway (NHO) kutoa mafunzo kwa wanawake ili waweze kushika za juu za
uongozi katika makampuni na taasisi mbali mbali ambapo tangu kuasisiwa kwake mwaka 2016, wanawake 66 wamehitimu mafunzo hayo.
Akiongea na wageni waalikwa, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jayne
Nyimbo Taylor alishukuru serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake katika kuboresha
mazingira ya kufanya biashara nchini kama punguzo la tozo
inayolipwa na waajiri kwa ajili ya kukuza ujuzi mahali pa kazi maarufu
kama “Skills Development Levy (SDL)” kutoka 6% mpaka kufikia 4.5% huku
akiiomba serikali kuipunguza tozo hiyo hadi kufikia 2%.
Pamoja na mapendekezo hayo, Bi.
Jayne Nyimbo pia aligusia changamoto mbali mbali zinazowakabili waajiri
kama ufuatiliaji wa vibali vya kufanya kazi nchini, utaratibu wa malipo
ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo sekta binafsi wanalipa 1%
huku waajiri wa umma wanalipa 0.5% ya mshahara anaolipwa mfanyakazi,
aina mikataba ya ajira pamoja na tozo na faini zinazotozwa na Mamlaka ya
Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA).
Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania(ATE), Dkt.
Aggrey K. Mlimuka, alitoa shukrani zake za dhati kwa Mgeni
Rasmi, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, wageni waalikwa na
wadau mbali mbali waliofanikisha Tuzo ya Mwajiri wa Mwaka 2018. “Naomba
nikushukuru tena Mhe. Mgeni Rasmi, na Washiriki wote kwa kuja kujumuika
na sisi katika utoaji wa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018, na naamini
kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa kushikiana na TUCTA pamoja na Serikali
hasa tunapoendelea kujenga nchi yetu kuelekea uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2025. Naomba kutumia fursa hii pia kuwashukuru na kuwapongeza
wanachama wote walioshiriki katika zoezi hili hasa kwa kujaza dodoso ili
kupata fursa ya kulinganisha utendaji wa makampuni yao na ya wengine.”
Alisema Dkt. Mlimuka.
“Naomba kuhitimisha salamu zangu kwa kuwatambua uwepo wa baadhi ya wanachama na
wadau wetu kwa michango yao ambayo imetuwezesha kufanikisha
utoaji wa tuzo hii ambao ni wafuatao.” Alimalizia Dkt. Mlimuka. Kuhusu
Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ni
chombo pekee cha waajiri
No comments:
Post a Comment