Wednesday, December 19, 2018

MKURUGENZI MKUU AAGIZA WATENDAJI NHC KUWAFIKIA WATEJA NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI ILI KUBORESHA HUDUMA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk. Maulidi Banyani akisikiliza maelezo ya Mhandisi wa NHC mkoa wa Kagera George Shannel wakati Mhandisi huyo akitoa ripoti ya mradi wa Muleba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,  Dk. Maulidi Banyani ametembelea miradi ya Bombambili Geita na Muleba mkoani Kagera na kushuhudia masuala mbalmbali

Akiwa Bombambili,  Geita alimuagiza Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza kuhakikisha kwamba nyumba hizo ambazo zimebaki 17 kupangishwa kati ya 38 kwa wakati na kwamba kati ya hizo nyumba 7 zinahitajika na Halmashauri. 

Meneja wa NHC Mwanza aliwasilisha ombi la kupangisha kwa shilingi 200 kwa  Mwezi, Mkurugenzi Mkuu aliwaagiza Mkoa na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki kuhakikisha wanawasilisha maombi hayo kwa barua. 

Hata hivyo ziliibuka changamoto nyingine ni kutokuwapo nondo za madirishani yaani grills kwaajili ya kuhakikisha usalama. 

Dk Banyani alisema inabidi suala  hili la grills lijadiliwe katika menejimenti ili liweze kutolewa msimamo.

Dk Banyani pia aliagiza Mameneja kupita kwa Wanunuzi walionunua ama kupanga katika nyumba mbalimbali na kisha kusikiliza maoni yao ili Shirika liweze kupata uzoefu kwaajili ya miradi mingine.

Naye Mhandisi wa NHC mkoa wa Kagera George Shannel akitoa ripoti ya mradi wa Muleba alisema kuwa mradi una nyumba 20 na kati ya hizo,  tatu zimenunuliwa,  16 zimepangishwa na moja inafanyiwa matengenezo.

Akizungumzia changamoto alisema ni suala la GRILL kwajili ya usalama na kwamba mpaka sasa nyumba zimewekwa tiles 16 kwa fedha za fungu la mkoa. 

Mkurugenzi Mkuu aliagiza iandikwe barua kwa Halmashauri kuelezea nia ya kuachia eneo ambalo halijalipwa fidia.



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk. Maulidi Banyani akisikiliza maelezo ya Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Kagera, Benith Masika wakati Mkurugenzi Mkuu alipotembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu Muleba mkoani Kagera. Nyumba za Makazi za Gharama nafuu Muleba zipo 20.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk. Maulidi Banyani akitoa maelekezo kwa watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (Hawapo pichani) alipokuwa katika ziara yake kwenye mikoa ya Geita na Kagera.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla akimsikiliza Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kagera , George Shannel walipokuwa katika ziara mkoani Kagera.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk. Maulidi Banyani akitembelea mradi wa Bombambili Geita.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk. Maulidi Banyani akimsikiliza mmoja wa wakazi wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa Bombambili Geita ambaye alimueleza Mkurugenzi Mkuu kuhusu kero ya maji inayowakabili katika eneo hilo jambo ambalo Mkurugenzi Mkuu aliahidi kulishughulikia.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Dk. Maulidi Banyani akimsikiliza Msimamizi wa Matengenezo wa nyumba za Geita ndugu Fadhili wakati alipotembelea nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa Bombambili Geita.
 Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa Bombambili Geita.


No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...