WAZIRI wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamja na Naibu Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Akson wakipokea vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.Anayewakabidhi vitabu hivyo ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mbeya bw, Bartholomew Masatu. Airtel imekabidhi vitabu hivyo mwishoni mwa wiki hii ikiwa ni ahadi yake ya kuendeleza masomo ya sayansi nchini.
WAZIRI wa Elimu Profesa, Joyce Ndalichako (Kushoto)akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania , Dkt.Tulia Akson , wakimkabidhi vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa sekondari ya Kayuki, Bertha Sarufu, vitabu vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. Mbali ya Kayuki, shule nyingine za sekondari zilizonufaika na msaada huo ni Ikuti, Bujela, Ntaba na Ikapu, zote zipo wilayani Rungwe.
Kampuni ya Simu ya Simu ya Airtel imekabidhi vitabu vya sayansi mwishoni mwa wiki vyenye thamani ya shilingi milioni 15.
Shule tano kufaidika na vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 5
Mbeya; Katika kuinua sekta ya elimu nchini , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa msaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa shule 5 za sekondari mkoani Mbeya.
Vitabu hivyo vimetolewa na Airtel kwa kushirikiana na Tulia Ackson foundation kwaajili ya shule za sekondari za Ikuti, Kayuki , Bujeli, Ntaba na Ikupa
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Naibu Spika Mh Dkt, Tulia Ackson alisema aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana na taasisi yake ya Tulia Ackson ili kusaidia shule za sekondari zenye uhaba wa nyenzo za kujifunzia mkoani Mbeya. Dr. Ackson alisema” ni muhimu kwa makapuni binafsi ya umma kushirikiana katika kuinua sekta ya elimu nchini ili kuweka mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi
Tumeshuhudia uhaba mkubwa wa vitabu katika mashule ambapo uwiano upo kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi 5 hadi 10. Tunaamini msaada huu tunaoutoa leo utasaidia kuzalisha nguvukazi yenye ueledi itakayowawezesha kujiajiri au kuajiriwa na kujenga uchumi wenye nguvu. Natoa wito kwa makapuni mbalimbali kuungana nasi na kuzifikia shule zenye uhitaji wa vifaa vya kufundishia nchini
Kwa upande wake Meneja Mauzo mkoani Mbeya, Bartholomew Masatu alisema” Airtel tunaamini jamaa iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vyakutosha hususani vitabu. Ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi hapa Mbeya”.
Tunaamini msaada utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa wetu.” Aliongeza Masatu
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa sekondari ya Kayuki Bi Bertha Sarufu Kwa niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu alisema “ Tunashukuru sana Airtel kwa kutufikishia msaada huu na napenda kutoa wito kwa wanafunzi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa lengo la kuboresha ufaulu. Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".
No comments:
Post a Comment