Wednesday, August 04, 2010

Mke wa Dk Slaa ahamia Chadema


ALIYEKUWA mgombea wa Ubunge wa jimbo la Hanang,kupitia CCM, Rose Kamili leo anatarajia kurejesha kadi ya CCM na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wilayani Hanang mkoani Manyara.

Kamili ambaye ni Diwani wa CCM tangu mwaka 1994 katika kata ya Basotu, alitangaza uamuzi huo, juzi mara baada ya kutangazwa matokeo ya Ubunge ambapo, yalionesha ameshindwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Mary Nagu.

Kamili ambaye ni mke wa Dk Slaa, mgombea wa Urais wa Chadema mwaka huu, alisema ameamua kujiondoa CCM kutokana na kutoridhishwa na mwenendo ya chama hicho hasa katika kampeni za ubunge.

"napenda kutangaza wazi kuwa mimi siwezi kumuunga mkono Nagu katika kampeni za ubunge na natarajia kurejesha kadi ya CCM kesho(leo)"alisema Kamili.

Kamili alisema ameamua kujiondoa CCM kutokaa na kutoridhishwa na uchaguzi huo, hasa kutokana na kitendo cha Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Michael Sakra kupiga kampeni wilaya nzima ashindwe.

"katibu amekuwa akiwaita viongozi wote wa CCM na kuwaagiza kuhakikisha Nagu anashinda wametumia fedha na hila nyingi hivyo nimeona basi mchango ambao nimeutoa CCM kwa zaidi a miaka 20 unatosha"alisema Kamili

Hata hivyo, alisema uamuzi wa kugombea ubunge au kutogombea atautangaza lakini anaimani chadema ina mgombea mwingine mzuri katika jimbo hilo.

Uamuzi wa kamili kujiunga na chadema utakuwa ni pigo kubwa kwa CCM Hanang na hasa kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo katika wilaya hiyo. Imeandikwa na Mussa Juma, Arusha: SOURCE MWANANCHI

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...