Tuesday, June 08, 2010
Mpigapicha Habari Leo amshukuru Rais Kikwete
MPIGA mpicha wa magazeti ya Serikali yanayochapisha magazeti ya Habari Leo na Dailynews (TSN), Athuman Hamisi amemshukuru Rais Jakaya Kikwete na uongozi wake kwa msaada mkubwa pindi alipokuwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kupata ajali mbaya mwaka 2008 na kusababisha ulemavu wa kudumu.
Hamisi aliyasema hayo jana mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari (Maelezo) wakati akizungumzia ajali ailiyoipata Septemba 12, mwaka 2008 katika eneo la Kibiti wakati akiwa njiani kuelekea Kilwa kikazi.
Alisema anamshukuru Rais Kikwete baada ya kwenda kujulia hali alipokuwa Muhimbili pamoja na Afrika Kusini alipokuwenda kwa ajili ya upasuaja mkubwa baada kuumia shingo na uti wa mgongo.
“Kweli hujafa hujaumbika huu ni usemi wa siku nyingi lakini siku ukimtokea kwako ndio unaona thamani ya msemo huo hali kadhalika kuwa hakuna barabara ndefu isiyokuwa na kona,” alisema Hamisi
Anasema kuwa baada ya ajali hiyo alipelekwa hospitali ya Muhimbili kitengo cha Mifupa Moi kwa siku 15 kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Hamisi ambaye kabla ya kuwa mlemavu alikuwa mpiga picha maarufu alisema kuwa Septemba 28, mwaka huo huo alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa upasuaji katika kipindi cha mwezi Oktoba na Novemba 2008 katika hospitali ya Millpark iliyopo mjini Johannesburg.
Alisema kuwa upasuaji wake ulichukua muda wa saa nane katika hospitali iyo iliyochini ya shirika la kimataifa la Netcare ambapo alikaa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa kipindi cha miezi mitano na wiki mbili kabla ya kuamia katika wodi ya nne ambayo ni ya wagonjwa wa kawaida.
Alisema kuwa upasuaji ulichelewa baada ya madaktari kuamua kutibu kwanza vidonda vya kichwani vilivyotokana na ajali hiyo.
Kwa sasa mimi naendelea vizuri ingawaje siwezi kusimama wala kutembea na baadhi ya viungo vyangu havifanyi kazi kutokana na kuvunjika kwa uti wa mgongo mpaka kiuno,”alisema Hamisi .
Alisema ni vigumu kuamini kwa watu waliomuona katika hospitali ya Muhimbili , Moi na siku alipoondoka kwenda Afrika ya Kusini kuni hali yake ilikuwa mbaya sana tofauti na sasa.
Hamisi aliwasili nchni Mei 8,mwaka huu kutoka Afrika ya Kusini alipokuwa kwa ajili ya matibabu yaliyodumu kwa zaidi ya miaka miwili.
Miongoni mwa matu wengine waliojeruhiwa katika ajili hiyo mwandishi ni Herry Makange ambaye kwa sasa ni marehemu baada ya kupata ajali ya pikipiki na Athony Siyame.
Vile vile ametoa shukrani kwa Wizara ya Afyana Ustawi wa Jamii, uongozi wa TSN, Ofisi ya Mawasiliamo Ikulu, pamoja na waandishi wa habari ikiwemo wadau wote kwa kwa sala zao pindi alipokuwa hospitali. Habari ya Hadija Jumanne. SOURCE: MWANANCHI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment