Mariam Migomba 'Mami' aibuka mtangazaji nyota




Hatimaye lile shindano la kumsaka mtangazaji bora wa vipindi vya taarab mwaka huu hapa nchini lilifikia tamati usiku wa siku ya Jumapili taehe 6/6/2010 ndani ya ukumbi wa hoteli ya Travertine, Magomeni jijini Dar ambapo mtangazaji nyota wa redio ya TBC1 Mariam Migomba 'Mami' aliibuka kidedea dhidi ya mtangazaji wa redio ya Times FM, Khadija Shaibu 'Dida'.
Katika mpambano huo ulioendeshwa kwa ustadi mkubwa na mtangazaji mwenzao Maimartha Jesse aliyekuwa MC, Mariam Migomba alipata kura 425 dhidi ya 386 za Dida ambapo pamoja na burudani ya kundi la Jahazi Modern Taarab mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Kinondoni, Mhe Idd Azzan.
Mratibu wa shindano hilo, Kaka Mwinyi, alisema kuwa, amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na shoo hiyo ambayo ilikwenda vizuri na kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi na mashabiki wa watangazaji hao waliokuwa na shauku ya kujua nani kati yao atatwaa taji la umalkia huo.
"Haikuwa kazi rahisi kuwakutanisha watangazaji hao katika jukwaa moja kwa dhumuni la kushindana, lakini, nashukuru Mungu mambo yalikwenda bara-bara na karibu kila aliyekuwemo ukumbini pale Travertine alionesha kuridhika na matokeo kwani hakukua na kuzomea wala kurusha chupa kama zilivyo shoo nyingine," akasema Kaka Mwinyi.
Aidha, katika shoo hiyo mbali ya washiriki hao kupata tuzo maalum zilizochongwa kwa nakshi kila mmoja, pia, walipata zawadi ya pesa taslim (kiasi hawakutaka kitajwe hadharani) walizokabidhiwa na Mbunge wa Kinondoni, Mheshimiwa Idd Azzan aliyekuwa Mgeni Rasmi wa shoo.
Wakati huo huo, Kaka Mwinyi amesema kuwa, baada ya shoo hiyo, anajipanga kufanya shoo kubwa zaidi na ya aina yake itakayohusisha watangazaji wote wa kike wa runinga na redio nchini kabla ya mwezi Desemba mwaka huu ili kuleta changamoto miongoni mwa wadau wa tasnia hiyo adhimu ya habari kwa njia ya redio na runinga.

brought to you by
kaka Mwinyi - 0713 552211 or 0655 002015 or 0777666888

Comments

Anonymous said…
moja kwa moja mariam migomba mami original abaki bingwa na mushabiki.mrembo wangu na mpenzi kwa mahaba yote
Anonymous said…
namuthamini na nitamupa iliyo haki yake mimi mwenzie Prince william kabwenze wa mashariki DRC